Fahamu kuhusu kitengo cha magonjwa ya dharura

 

Magonjwa ya dharura ni yale magonjwa yanayohitaji matibabu ya haraka katika kipindi cha muda mfupi ili kuokoa maisha, kupunguza maumivu au kutoa tiba ya awali. Mara nyingi huhusishwa na ajali ambazo hutokea sehemu mbalimbali kama barabarani au nyumbani.

Baadhi ya magonjwa ya dharura ni kama mshituko(shock), kushindwa kupumua, kupata maumivu makali ya kifua, maumivu/uchungu wa kutaka kujifungua, kunywa sumu, kuvunjika, kuungua mwili, pumu (asthma) na mengineyo.

Kitengo cha magonjwa ya dharura ni kati ya vitengo muhimu katika hospitali, kwa Tanzania kitengo hiki kinapatikana katika hospitali za rufaa na hospitali ya Taifa.

Ukifika katika kitengo cha magonjwa ya dharura ni vema kuelezea tatizo au dharura uliyonayo au aliyonayo uliyekuja nae ili kuharakisha utolewaji wa huduma.

Kimegawanyika kutokana na huduma ambazo zinatolewa 1.Kitengo kinachopokea wagonjwa wanaohitaji huduma muda huo huo(immediate intervention) 2.Kitengo kinachopokea wagonjwa wanaohitaji huduma ndani ya dakika kumi(urgent cases) 3.kitengo kinachopokea wagonjwa wanaohitaji huduma badaa ya masaa kadhaa(Acute cases).

Vitengo vyote hivyo hutegemea kitengo kiitwacho (triage) ambacho wagonjwa hufika na kufanyiwa uchunguzi wa haraka kabla ya kupelekwa katika sehemu za kuwanusuru maisha, kuwapa matibabu zaidi au katika wodi za kulazwa na kuendelea kupata matibabu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show