Namna ya kujifanyia uchunguzi wa saratani ya matiti

 

1. Lala chali kwenye kitanda kisha weka mkono wa kushoto chini ya kichwa na tumia mkono wa kulia kuchunguza titi la kushoto. Kwa kutumia vidole vyako vitatu, chunguza titi kwa kubinya, ukizunguka titi zima. Angalia kama unaweza hisi kitu kigumu au utofauti sehemu yoyote ya titi kwa kutumia vidole vyako. Fanya hivyo hivyo kwa titi la kulia ukitumia mkono wa kushoto

2. Angalia matiti yako ukiwa umesimama mbele ya kioo na umeweka mkono kiunoni. Angalia kama unaona tofauti ya ukubwa, rangi ya ngozi, uvimbe au kubonyea kwa sehemu moja ya titi

3. Nyanyua mkono wa kushoto kisha tumia mkono wa kulia kujichunguza chini ya kwapa la kushoto. Angalia kama unaweza hisi uvimbe kwa kutumia vidole vya mkono wako. Fanya hivyo hivyo kwa kwapa la kulia.

4. Kwa kutumia vidole vyako vya mkono wa kulia, binya chuchu za titi la kushoto na angalia kama kuna maji maji au kitu chochote kinatoka kwenye chuchu. Fanya hivyo hivyo kwa titi la kulia.

Uchunguzi huu yapasa ufanyike angalau mara moja kila mwezi. Na endapo utahisi uvimbe (kitu kigumu) kwenye titi au kwapa, kubadilikwa kwa rangi au ukubwa wa titi, au kutoka kwa maji maji, damu au kitu chochote kwenye chuchu za titi. Haraka, nenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi na vipimo zaidi kwani hizo ni dalili za awali za saratani ya titi. Saratani ya titi inatibika kabisa kama ukiwahi mapema hospitalini kwa matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show