UHUSIANO KATI YA KIMEO NA AFYA YA MTOTO

‘’Mtoto wangu anakohoa sana nimehangaika kutafuta dawa imeshindikana,jirani yangu alinipeleka mahali wakamkata mwanangu KIMEO!..Lakini tangu alipokatwa  mwanangu amekuwa mnyonge anashindwa kucheza na wenzake  na kikohozi hakijaisha’’ alisimulia mama mwenye mtoto aliyekuwa na upungufu mkubwa wa damu alipofika ofisini kwa daktari.

Madaktari hukutana na malalamiko kama haya kutoka kwa wazazi ambao kwa bahati mbaya walipotoshwa na dhana ya KIMEO..Leo tutaangalia kimeo ni nini,na je kinatakiwa kikatwe? Je kuna uhusiano wowote na afya ya mtoto?..

Kimeo(uvula) ni moja kati ya misuli laini inayotengeneza sehemu ya koo watu wengine hukiita kidaka tonge au kilimi,kumekuwa na dhana potofu ya kuwa kimeo kinaweza kuleta matatizo kwa afya ya mtoto kama

 • Kukohoa sana
 • Kutokukua vizuri kwa mtoto au kudumaa
 • Wengine wanafikiri mtoto anaweza kukimeza na kufariki
 • Kimeo kirefu huleta maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji wa mtoto.

Zifuatazo ni hatari na madhara yanayoweza kutokea kama kimeo kitakatwa hasa kwa waganga wa kienyeji.

 • Maumivu makali maana hawatumii ganzi hii yaweza kumfanya mtoto au anayekatwa kulia sana na baadaye kukataa chakula au kushinwa kumeza chakula.
 • Kupata maambukizi mbalimbali kama ugonjwa wa UKIMWI,tetenasi,kifua kikuu,homa ya ini na magonjwa mengine mengi ya kuambukiza.
 • Kupoteza damu nyingi
 • Kifo endapo kimeo kitaangukia kwenye koo la hewa maana waganga hawana vifaa maalumu vya kukishika wanapokikata.
 • Kusababisha baadhi ya maeneo ya koo kukosa damu kwa muda mrefu hvo kupata iskemia
 • Kuharibika kwa sehemu ya juu ya koo hivo kusababisha matatizo wakati wa kuongea pia chakula na maji kutokea puani .

Ukweli ni kwamba kitaalamu hakuna uhusiano wowote kati ya kimeo na haya yanayozungumzwa mitaani,ingawa zipo sababu chache sana ambazo zinaweza kupelekea kukatwa kwa kimeo kitaalamu mfano wengine huzaliwa na kimeo kirefu kuliko kawaida,maambukizi sugu kwenye kimeo na koo lakini haya yote ni lazima yawe yamechunguzwa kwa kina na madaktari na wakajiridhisha kuwa hakuna njia nyingine ya matibabu zaidi ya kukikata hivo usikubali mwanao akakatwa kimeo wala wewe mwenywe bila kuwa umeshauriwa na daktari na huduma hiyo ifanyike hospitalini na si mahala pengine.

 

 

7 thoughts on “UHUSIANO KATI YA KIMEO NA AFYA YA MTOTO

  1. Asante paul kwa swali zuri.Dawa za meno zipo za aina nyingi ila vya kuzingatia ni kutumia dawa yenye madini ya floridi{fluoride} na kuepuka kununua dawa zilizoandikwa kuwa zinanga’arisha meno na kuyafanya meupe. Dawa kama Colgate na whitedent ndio zinazoshauriwa kutumika.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show