Dhana potofu meno ya plastiki

Dhana ya meno ya plastiki ni maarufu katika nchi za ulimwengu wa tatu na Tanzania ikiwemo,dhana hii imekuwa ikiwapa wasiwasi wazazi wengi.Je ukweli ni upi?

Mtoto anapofikia umri wa kouta meno fizi huvimba na mara nyingi vijitoto vya meno(tooth buds) huonekana ndani ya fizi katika maeneo ambayo meno hutokea baadae.Watu wengi wakiwemo wazazi wamekua wakiamini yanasababisha kutapika ,kuharisha na homa kwa mtoto na hivyo huamua kuyatoa.

  • Dhana hii potofu imesababisha watoto wengi wenye umri wa miezi 6 hadi 24 kutolewa meno haya wakidai ni minyoo ndani ya meno na kuwa kuyatoa ndo suluhisho pekee la mtoto kupona.Utafiti unaonyesha kuwa waganga wa jadi ndio wanaosambaza habari hizi na kuleta hofu kwa wazazi kwamba meno hayo yasipotolewa huweza kusababisha kifo cha mtoto.

Vijimeno hivi huonekana kwenye fizi kama uvimbe wa rangi nyeupe na unaong’aa.

Vijimeno hivi huonekana kwenye fizi kama uvimbe wa rangi nyeupe.
  • Meno haya yakitolewa yanakua hayajapata madini ya kutosha na huwa malaini ndo maana huitwa “meno ya plastiki”.

Nini madhara/harasa endapo meno haya yatatolewa?

  • maumivu makati kwa mtoto kwani waganga hawatumii ganzi
  • magonnjwa ya kuambukiza kama HIVn na homa ya ini maana vifaa vinavyotumika huwa si salama.

Vijimeno hivi vinaeza kutolewa vyote au nusu nusu.

  • Vikitolewa vyote mtoto atakosa kabisa meno haya mdomoni na vikitolewa nusu jino bovu huota hapo baadae.
husababisha kuharibika kwa meno au kukosekana kwa meno hayo apo baadaye.
  • Pia katika kutoa vijimeno hivi meno ya pembeni yanaweza kudhurika na hata kuota vibaya hapo baadae

Hivyo basi vijimeno hivi havitakiwi kutolewa maana havina uhusiano wowote na mtoto kuumwa bali viko pale kama ishara ya meno yataotoka mdomoni.Elimu kubwa inahitajika kwa jamii ili kuondoa imani hii potofu na kutunza afya ya kinywa na meno ya watoto wetu.Kuwa balozi wa kupeleka elimu sahihi kwa jamii jifunze kila siku kuhusu mambo yanayojadiliwa mtaani na jua ukweli.

 

 

13 thoughts on “Dhana potofu meno ya plastiki

      1. Dr. Unachoongelea Ni Sahihi Kipo Kwenye Jamii, Na Unasema Visitolewe Na Kama Havitolewi Anakufa! Sasa Suluhisho Ni Lipi?

  1. Jamani hayo meno yanayosemekana niyaplastic miongoni mwa jamii inasadikiwa kwamba huwa wanaenda Kwa waganga wa kienyeji kuyatoa (tooth pula), hivyo basi tunapaswa kutoa elimu sana hasa sehemu za vijijini maana Mara nyingine wanasababisha magogongwa yasiolazima Kwa mtoto. Tufanye Sana uelimishaji mashuleni, RCH, monthly babies clinic, and HBC programs. Tukifanya hivyo tutawasaidia kids wetu ambao nitaifa lakesho

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show