Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeng’atwa na nyoka

Nyoka ni wanyama ambao ni hatari hasa pale wanapomg’ata mtu, lakini kuna uwezekano nyoka akawa mwenye sumu au asiwe mwenye sumu. Endapo nyoka aliyehusika akawa mwenye sumu basi chukua tahadhari, kwani huweza kusababisha kifo papo hapo au baada ya mda. Mtu aliyeng’atwa na nyoka anahitaji kuwahishwa kwenye kituo cha afya au hospitali haraka!

Ila wakati utaratibu wa kumpeleka hospitali ukifanyika ni muhimu sana kumpa huduma ya kwanza kama ifuatavyo:

 • Kwanza kabisa jitahidi utambue muonekano wa nyoka huyo kama ameonekana ili uweze kuelezea kwa wataalamu wa afya.
 • Kisha mtulize mwathirika asihangaike wala kutembea tembea, mlaze chali na hakikisha asiinue sehemu alipong’atwa juu zaidi ya usawa wa moyo. Hii itasaidia kupunguza sumu kusambaa mwilini.
 • Pia muondole wasiwasi ili kupunguza msukumo wa damu unaoweza kupelekea usambazwaji wa sumu husika mwilini kwa kiwango kikubwa.
 • Ondoa vitu vinavyobana kama pete au nguo za kubana kwenye sehemu iliyong’atwa kwani sehemu hiyo inaweza kuvimba.
 • Usifunge sehemu ya juu au chini ya alipong’atwa kwa nguo, kamba au kitu chochote kile kingine.
 • Usikate au kupasua sehemu iliyong’atwa kwa kisu au kiwembe  na pia usijaribu kunyonya sumu kutoka kwenye sehemu iliyong’atwa kwa mdomo.
 • Usimpe kitu chochote cha kula wala usiweke barafu kwenye sehemu iliyong’atwa.
 • Pia angalia hali ya mgonjwa: mapigo ya moyo, upumuaji na joto la mwili. Kama anakuwa wa baridi mfunike ili aweze kupata joto.
 • Muwahishe kituo cha afya au hospitali iliyo karibu na wewe kwa ajili ya matibabu. Kama  nyoka aliyemng’ata yupo aliuliwa au kukamatwa, nenda naye katika kituo cha afya au hospitali pia.

15 thoughts on “Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeng’atwa na nyoka

  1. Asante sana kwa swali lako, kwanza kwa kuangalia maumbile ya nyoka unaweza kumtambua nyoka mwenye sumu, kwani asilimia kubwa ya nyoka wenye sumu huwa na: kichwa chenye pembe tatu, wenye rangi za kung’aa au rangi nyingi tofauti, macho yaliyochongoka kama ya paka, pia wenye mkia unaokuwa unatetemeka(rattle). Wakati kimaumbile asilimia kubwa ya nyoka wasio na sumu huwa na: kichwa cha kama mviringo, wasio na rangi za kung’aa na wenye macho ya mviringo. Lakini pia tabia, kwa mfano nyoka wa kwenye maji amabao huogelea huku mwili wote ukiwa unaelea juu ya maji wana sumu. Mwisho kwa kuchunguza sehemu iliyong’atwa, kama utaona alama mbili (kama vitundu) hii inaashiria meno mawili amabayo nyoka wenye sumu hutumia kutoa sumu, wakati kama sehem iliyong’atwa haina alama hizi mbili zikionekana vizuri hii huashiria kung’atwa na nyoka wasio na sumu.

   1. Shukrani dr kwa hapo nina hakika nimetoka na kitu ambacho kimeongeza ufahamu wangu wa namna ya kukabiliana na nyoka wenye sumu.

    Muendelee kutuhabarisha zaidi

  1. Ni muhimu sana kuhakikisha unamfikisha muathirika kwa haraka katika kituo cha afya au hospitali, kwani hata baada ya kumpatia huduma hii ya kwanza muathirika huitaji kupewa dawa(antitoxin) ambazo hutumika kuzuia madhara ya sumu ya nyoka mwilini pamoja na matibabu mengine muhimu. Endapo atakosa kufikishwa katika kituo cha afya au hospitali basi sumu itamsababishia madhara muathirika. Lakini pia ukali wa sumu hutofautiana, kwa mfano nyoka wenye sumu kali kama fira(cobra) na koboko(black mamba) huua ndani ya dakika ishirini(20) tuh baada ya kumng’ata mtu na kama mtu huyu hakufanikiwa kuweza kufika hospitali mapema kwa ajili ya kupata dawa(antitoxin).

 1. Usifunge sehemu ya juu au chini ya alipong’atwa kwa nguo, kamba au kitu chochote kile kingine.

  Hii haiwezi kusababisha sumu kusambaa kwa kasi,,, nilihis kufunga kutasaidia kuopunguza usambaaji wa sumu,..?

  1. Haishauriwi kumfunga muathirika nguo au kamba sehemu ya juu au chini ya alipong’atwa, kwani kitendo hiki cha kumfunga kitaathiri mzunguko wa damu na kusababisha damu kutokufika pamoja na kutokutoka sehemu hyo kama kawaida. Damu ya kutosha isipo fika sehemu hiyo basi seli na tishu zitakosa oksijeni na virutubisho muhimu na hii itapelekea seli na tishu za sehemu hiyo kufa na kusababisha madhara makubwa zaidi. Kwa mfano muathirika aliyeng’atwa na nyoka sehemu ya mguu na akafungwa mguu huo kwa kamba, utasababisha mguu huo ukose mzunguko muhimu wa damu hivyo seli na tishu za mguu zitakufa. Na kutokana na seli na tishu kufa hii itapelekea madhara makubwa zaidi ya kukatwa mguu wote kabisa.

 2. Daaah hili jambo lilikuwa halifahamiki vizur kabisa yaan MTU alikuwa aking’atwa na nyoka au ng’e anafunga sehem ya juu yake ili damu isisambae mbali

  Ila na mm nauliza usipomfunga kamba damu si itasambaa sana kwenye mzunguko wake na kusababisha madhara makubwa sana na kuna baadhi ya nyoka wana affect CNS maelezo apo Dr!!!

  1. Asante kwa swali lako la nyiongeza. Kwa kuanzia, damu ilikukamilisha mzunguko mmoja mwili mzima na kisha kurudi kwenye moja kwaajili ya kuanza mzunguko mwingine huchukua takribani dakika moja tuh. Na mara nyingi mpaka mtu huyo aje kufungwa kamba sehemu hiyo huweza kuchukua dakika kadha au mda mrefu zaidi ya huo. Hivyo sumu huwa ishasamba mwilini kwani damu huwa tayari imesha kamilisha mzunguko wake. Lakini pia endapo kama utaweza kuwahi na kupafunga kamba kwa haraka kabla damu haijakamilisha mzunguko wake, kwa kufanya hivyo utakuwa umeilundika sumu yote sehemu moja katika eneo hilo la mwili ulipoifungia, na wote tunafahamu kuwa sumu hizi huwa ni kali, na sasa yote ipo sehemu moja hivyo atahari itakayotokea katika eneo hilo itakuwa ni mbaya sana. Athari itakuwa na unafuu kidogo pale ambapo sumu itazunguka kwenye damu nyingi kwani kwa kiasi itakuwa imepunguzwa makali. Mwisho kabisa ni muhimu kumfikisha muathirika haraka katika kituo cha afya au hospitali iliyo karibu kwaajili ya kupata dawa aina ya antitoxin na huduma zaidi ilikuweza kuokoa maisha ya muathirika.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show