Kuelekea kufikia malengo yangu ya mazoezi(part 1)

 

Mazoezi ni muhimu kwa afya pale yanapofanywa mara kwa mara na kwa usahihi. Mazoezi yatakufanya mwenye nguvu Zaidi na kurefusha maisha. Ikiwa unafanyia mazoezi yako nyumbani, mahali pa nje ama gym, kuna vitu muhimu vya kufanya ili mazoezi yawe yenye matokeo yanayotarajiwa.

Vitu hivi huanzia kwenye maandalizi kabla ya kuanza mazoezini mpaka mazoezi yenyewe. Kwenye Makala hii nitaelezea sehemu ya mwanzo yaani maandalizi kati ya zile nyingi na muendelezo utakuwa katika Makala zitakazo fuatia.

Vifuatavyo ni vitu muhimu katika sehemu ya maandalizi. Kama ifahamikavyo kuwa katika hali nyingine  mwanzo  huwa ni mgumu ila unapofanikiwa mazoezi huwa yenye furaha;

 1. Vaa nguo sahihi za mazoezi ,zisizobana hasa katika maeneo ya jointi wala zile zinazothibiti kujitanua kwa mwili vya kutosha.
 2. Vaa raba sahihi, zinavokutosha vizuri, nyepesi na inashauriwa zenye soli pana
 3. raba zenye soli pana na nguo zenye nafasi
 4. Kunywa maji ya kutosha kabla ya kufanya mazoezi ,maji yatakusaidia katika kutanuka kwa misuli kipindi cha mazoezi na pia kuondoa harufu mbaya ya jasho.
 5. Usijinyooshe(stretching) kabla ya kuanza mazoezi hii ni kinyume na wengi waaminivyo .ila kujinyoosha kunaweza kuchosha misuli yako hata kabla ya mazoezi.
 6. Fanya mazoezi ya kupasha ,haya ni sawa kabisa na mazoezi unayoapanga kufanya ila unayafanya kwa nguvu ndogo Zaidi. Kwa mfano ;ukipanga kukimbia utaanza kwa kukimbia kwa spidi ndogo (jogging) halafu ndipo utaongeza mwendo.
 7. Uwe na malengo ya aidha kila wiki au kila mwezi ya matokeo yatokanayo na mazoezi unayofanya.
 8. Fanya mazoezi yanayokupa furaha na motisha Zaidi.
 9. Fanya mazoezi yatakayokuwa yanachangamsha sehemu nyingi za mwili wako.
 10. Onana na daktari kama una matatizo ya kiafya kama magonjwa ya pumu, mapafu, figo ,moyo na kadhakika, hii itakusaidia kupata ushauri sahihi wa aina ya mazoezi yanayoweza kufaa kulingana na hali yako. Vivyohivyo kama unapata shida wakati wa mazoezi kama kuishiwa pumzi ama kuchoka sana ,kuonana na daktari itakusaidia kujua hali yako ya afya na kuepusha magonjwa.

Iwapo ukiweza kufanya maandalizi mazuri, mazoezi yako yataenda vyema na hata kupata matokeo mazuri bila ya kuchoka wala kujiumiza. Tukutane wiki ijayo tukizungumza aina tofauti za mazoezi na faida zake mwilini.

 

4 thoughts on “Kuelekea kufikia malengo yangu ya mazoezi(part 1)

 1. Shukrani kwa maelezo ya mwanzo juu ya mazoezi, mie nina maswali manne:

  1. Je ni mavazi yapi ni sahihi kimazoezi, yale ya wazi (kama bukta na singlendi) au yanayofunika (kama track shit na masweta au jackets)?

  2. Vipi kuhusu uvaaji wa raba za soli pana, kwanini inashauriwa hivyo?

  3. Je unywaji wa maji kabla ya mazoezi hauwezi kusababisha kujaza tumbo na kupunguza ufanisi wa mazoezi?

  4. Je kwanini inazuiliwa kujinyoosha kabla ya kuanza mazoezi?

  Ni hayo tu kwa leo…

  1. Asante sana kaka kwa maswali;1.mara nyingi mavazi hutegemea na mtu mwenyewe na mahala anapofanyia mazoezi kama mtu huhisi joto zaidi akiwa nje anaeza penda mavazi mepesi vyivyo hivyo ikiwa ndani na hali kadhalika na mapendeleo ya mtu ili hali zisibane joint na zile zenye kuruhusu misuli kutanuka.
   2.viatu vya soli pana yaani vyenye kulingana na upana wa mguu wa mtu na sio virefu maana vinaweza sababisha kuumia
   3.kuhusu maji inabidi iwe tabia ya mtu wa mazoezi kunywa maji ya kutosha na hasa saa moja mpaka mawili kabla ya kuanzia mazoezi na endapo ni katika tu ya mazoezi unakunywa maji kidogo tu kwa kila dakika 15 na ni maji kidogo tu sio mengi.
   4.kujinyoosha hii tunaita stretching mara nyingi huweza kumfanya mtu a choke hata kabla ya kuanza mazoezi na baadae a yake tunashauri afanye mazoezi Yale anayopanga fanya kwa nguvu kidogo na kuongeza pole pole.
   Asante sana natumaini nimekujibu iwapo kuna maswali zaidi usisite kuuliza.

 2. Asante sana kwa elimu hii uliyotupatia ningependa kujua madhara ya kuanza mazoezi afu kuyaacha baada ya mda je ni kwel kua kuna kua na matokeo mabaya Kama kuumia sana kwa viungo na pia mwili kurudia hali yake ya mwanzo na ata kuzidi pale

 3. Nashukuru kwa swali ni kawaida ya misuli na viungo vya mwili kuuma pale vinaponyooshwa zaidi katika mazoezi kutoka kwenye hali ya ukawaida wake!hivyo ni vyema kuuendelea kufanya mazoezi ili kuuzoesha mwili.
  Ni kweli kuwa mtu anapoacha mazoezi anaweza rudia hali ya mwanzo kwa maana mwili utarelax na uwezekano wa hata kuzidi huja pale anapokuwa anakula vyakula visivyo na afya zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show