Endometriosis

Endometriosis ni hali ambayo seli za mfuko wa uzazi huota sehemu nyingine mbali na ukuta wa uzazi. Hizi seli zilizoota sehemu nyingine, hujaribu kufanya kazi kama seli za ukuta wa uzazi zinavyofanya kazi. Seli hizi mara nyingi huota sehemu zifuatazo.
i) ovari za mwanamke
ii) mirija ya Fallopian
ii) mirija ya mkojo.
Visababishi vya hali hii havijulikani. Kuna baadhi ya watu wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa huu, na hivi ni baadhi ya vitu hatarishi ambavyo humuweka mtu katika hatari ya kupata endometriosis,
1: Uwepo wa mwanafamilia mwenye endometriosis
2: Kuanza hedhi mapema
3: Kuwa na mzunguko wa hedhi mfupi ( siku chini ya 21)
4: Kuwa na hedhi nzito inayotoka kwa siku zaidi ya saba
5: Kuchelewa kuzaa
Haimaanishi kwamba vitu hivi huonesha kuwa mtu ana endometriosis, bali humaanisha mtu huyu yupo katika hatari ya kupata endometriosis ukilinganisha na wale ambao hawana hali hiyo.
Zifuatazo ni dalili za ugonjwa huu.
1: Kuwa na maumivu makali kipindi cha hedhi hasa hasa maumivu ya kiuno
2: Kuwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa
3: Ugumba
4: Kupata maumivu wakati wa haja kubwa na ndogo

7 thoughts on “Endometriosis

 1. Mwanamke mwenye endometriosis ana nafas ya kupata ujauzito kama wanawake wengine Au akishakuwa na tatizo ndio mtu hawezi kuzaa tena?

  1. Mwanamke mwenye endometriosis hawezi kupata ujauzito kabisa, yaani nakua mgumba. Na pia watu wenye ugumba wanashuriwa kuangalia vipimo vya endometriosis kwa sababu ipo kati ya dalili za endometriosis.
   Lakini pia hata watu wenye ugumba wanaweza kusaidiwa kupata watoto kwa njia inayoitwa In Vitro Fertilization (IVF)

  2. Kuna mwanadada anaitwa Millen Magese, aliwahi kushindania tuzo za Miss Tanzania miaka ya nyuma. Yeye ni mmojawapo ya wanawake wenye ugonjwa huu na alihangaika nao sana mpaka akaanzisha movement ya kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa huu. Miaka ya hivi karibuni amefanikiwa kupata mtoto wa kiume. Unaweza kufuatilia historia yake utaelewa zaidi kuhusu ugonjwa huu maana ametumia uzoefu wake binafsi

  1. Epuka vitu hatarishi nilivovitaja hapo juu.
   Kwa watu wenye maumivu makali wakati wa hedhi inashauriwa watumie dawa za kupunguza maumivu
   Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kupunguza kiwango cha hormone zilizozidi
   Pia fika kwenye kituo cha afya kama unavitu hatarishi ili kupata uangalizi wa karibu

  1. Tiba ya ugonjwa huu umegawanyika katika sehemu mbili
   Tiba kwa njia ya kurekebisha homoni na tiba kwa upasuaji.
   Katika upasuaji endapo mtu atawahi kuugundua anaweza kutoa sehemu iliyo athirika tu na akaweza kutunga mimba. Ila pia kutolewa kwa kizazi chote endapo njia tajwa hapo juu hazitasaidia

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show