Homa ya Ini (dalili na njia ya usambazaji)

Homa ya ini ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha aina ya hepatitis virus. Homa hii inaweza kusababishwa na kirusi cha aina A, B, C, D au E.

1. Homa ya Ini Ina Dalili Zipi?

Dalili ni:

  • maumivu makali ya tumbo la juu upande wa kulia
  • kukosa hamu ya kula
  • homa za mara kwa mara
  • macho kuwa ya njano
  • mkojo kuwa mweusi
  • kupungua uzito kwa ghafla

endapo utaona dalili hizi, ni vyema kufika katika kituo cha afya kuonana na mhudumu wa afya.

2. Kirusi hiki husambazwa kwa njia zipi?

Njia tofauti hasa kwa njia za majimaji ya 
mwili huongoza katika usambazaji wa virusi hivi. 
Njia hizi ni kama:
  1. Kupitia mate. Mate ya mtu mwenye homa ya ini hubeba virusi hivi. Hivyo inapotokea mtu mwingine akayagusa kwa njia yoyote anaweza kuambukizwa.
  2. Kupitia majimaji ya sehemu za siri. Watu wanapo jamiiana bila kinga, inaweza kusambaza ugonjwa huu. Hivyo kuwa na wapenzi wengi kunamuweka mtu kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu.
  3. Damu ambayo inavirusi hivi husambaza homa ya ini kwa haraka zaidi. Hivyo ni sahihi zaidi kujiepusha kugusa damu ya mtu mwingine.

1 thought on “Homa ya Ini (dalili na njia ya usambazaji)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show