Ningependa kupona Kisukari kabisa (Part 2)

Kubadilisha hali yako ya kisukari siyo jambo linaloweza kutokea ndani ya usiku mmoja. Inahitaji malengo na kujituma na hii itakusaidia kupunguza uwezekano wa matatizo yatokanayo na kisukari. Kudumisha kiwango cha sukari cha kawaida kwenye damu ambacho ni;

 • 4-6 mmol/l ikiwa hujala masaa 8 au zaidi au
 • 7.8 mmol/l au chini ya hapo ikiwa ni muda wowote au masaa mawili baada ya kula.

Njia zipi sasa nitumie!?

 

1. Matumizi ya mlo wenye kiasi kidogo cha wanga
Huu ni ule mpango mzima wa uchaguzi wa chakula kutoka kwenye yale makundi ya vyakula kulingana na upatikanaji na jinsi ya kupima chakula chako kama ilivoelezewa kwenye makala ya  http://daktarimkononi.com/2018/02/11/nile-nini-endapo-nina-kisukari-part-2/

2. Matumizi ya mlo wenye kiasi kidogo cha kalori
Mlo wenye kiasi kidogo cha kalori mara nyingi hutumika ili kumsaidia mtu kupunguza uzito kwa kilo 0.5-0.9 ndani ya wiki moja. Hii huwa inajumuisha kupunguza kiasi cha mafuta kwa zaidi ya 20-35% ya kiasi chote cha kalori unachotumia, kula wanga mchanganyiko kama vile nafaka zisizokobolewa, mbogamboga na matunda, kutumia protini zenye kiwango kidogo cha mafuta kama samaki, kuku, mimea jamii ya kunde (maharage, njegere, njugu), vyakula vyenye kambakamba (fibres).
Ulaji huu unahitaji vipimo maalumu kwa kila aina ya chakula na unahitaji usimamizi wa mtaalamu hasa wa lishe ili kuzuia mtu asipate lishe duni.

3. Upasuaji (Bariatric Surgery)
Hii inahusisha upasuaji unaopunguza kiasi cha chakula kinachoweza kubebwa na tumbo au kuzuia umeng’enywaji mzuri wa chakula na kupelekea kupunguza uzito na kupunguza uwezekano wa kupata athari za kisukari. Hata hivyo hii inatakiwa kuwa njia ya mwisho kuifikiria.

“muhimu unatakiwa kujua kwamba kisukari huwa hakisubiri, usipofanya kitu chenyewe kinaendelea”

2 thoughts on “Ningependa kupona Kisukari kabisa (Part 2)

 1. Shukrani daktari, nimejifunza jambo kubwa sana kuhusu kisukari…

  Nilikuwa sifahamu kwamba mgonjwa wa kisukari anatakiwa kupungua uzito, je ni kwanini?

  1. Asante kwa kujifunza
   Kuwa na uzito mkubwa unaotokana na kulundikana kwa mafuta mwilini huhusishwa na muingiliano wa kazi wa insulin(homoni inayosaidia kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu) au kitaalamu husemwa kama “insulin resistance”
   Tunashauri mtu mwenye kisukari kupunguza uzito ili kuongeza uwezo wa insulin kufanya kazi yake na hivyo kufanya urahisi wa kurekebisha kiwango cha sukari.
   Endelea kujifunza zaidi na Daktari Mkononi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show