Mtoto wangu ana kisukari lakini tabia yake siielewi

Mtoto wako kuna wakati anakukasirisha; kitu ambacho watoto wengi hufanya lakini kabla ya kumuadhibu unajiuliza kwanza “je amefanya hivi makusudi, ni sukari yake imepanda au imeshuka!?”

Haya ni maswali ambayo wazazi wa watoto wenye kisukari hujiuliza mara tabia za watoto wao zinapobadilika. Kisukari hufanya hali ya kulea watoto kuwa ngumu kwa kuwa inahitaji umakini kutambua na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya mtoto wako.

Ni muhimu kubaini kwamba tabia ya wakati fulani kama ni matokeo ya mabadiliko ya kiwango cha sukari au la. Tabia hizi kulingana na kiwango cha sukari ni kama;

  • Sukari kushuka kwenye damu (Hypoglycemia)

Mtoto huonesha dalili kama kubadilika kwa hisia (mood), kutotulia, kuwa na tabia zisizofaa au hata ukatili. Mzazi aliyezoea hali ya sukari ya mwanaye aonapo dalili hizi mara moja humsaidia kwa kumpa kitu chenye sukari ili kuongeza kiwango cha sukari.

  • Sukari kupanda kwenye damu (Hyperglycemia)

Hapa mtoto huonesha dalili kama mwili kuchoka, kupoteza umakini, kichefuchafu, maumivu ya kichwa. Ukiona hali hii mtoto anatakiwa apatiwe insulin, anywe maji au afanye mazoezi mara moja ili kupunguza kiwango cha sukari.

“Dalili hizi mara nyingi huwa zinachanganya na siyo rahisi kuzitofautisha hivyo basi mzazi uonapo mabadiliko ya tabia ya mtoto wako ni vyema kupima kiwango chake cha sukari kwenye damu.

2 thoughts on “Mtoto wangu ana kisukari lakini tabia yake siielewi

  1. Shukrani kwa darasa la bure….

    Kwa tabia hizi je ni busara mzazi kukaa mbali na mtoto maana akipatwa na hizo dalili akiwa anacheza si hatari?

    1. Ni hatari kweli endapo mtoto atapata dalili hizo akiwa mbali na mzazi wake kwa kuwa anaweza asipate msaada wa haraka. Wakati huo huo mtoto hatakiwi kukatazwa kucheza kwa sababu ni muhimu katika ukuaji wake; Ndiyo maana rafiki yake wa karibu anatakiwa ajue kuhusu ugonjwa wake ili iwe rahisi kupata msaada anapokua mbali na mazingira ya nyumbani.
      Nashukuru sana kwa kuzidi kutembelea Daktari Mkononi, tafadhali usichoke kusoma na kuwashirikisha wengine

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show