Usugu wa madawa

Usugu wa madawa ni nini?
Usugu wa madawa ni hali ya dawa kushindwa kuua au kuzuia ukuaji wa vimelea vya magonjwa.
Vimelea hivyo ndivyo hujenga usugu wa dawa.
Dawa zipi zinaathiriwa?
Dawa zote zinazotumika kutibu magonjwa ya kuambukiza huweza kuathiri usugu wa dawa. Mfano wa dawa zinazotumika mara kwa mara ni ciprofloxacin (cipro), metronidazole (flagyl) na amoxicillin ndo zinaathiriwa zaidi.
Nini kinasababisha usugu wa dawa?
• Matumizi ya dawa kama antibayotiki kwa muda mrefu.
• Ujuzi hafifu wa watoa dawa (kutokuijua dawa vizuri na matumizi yake).
• Kutokutumia dozi sahihi ya dawa na kwa muda ulioelekezwa.
• Kutokutumia dawa sahihi dhidi ya ugonjwa ulionao.
• Kutumia dawa zinazokinzana kiutendaji.
• Kunywa pombe wakati wa kutumia dawa.
• Kukatisha dozi mara baada ya kupata nafuu.
• Kutumia dawa bila ya kufanya vipimo.
• Kuuza dawa kwa lengo la kupata faida bila ya kujali afya ya mgonjwa.
• Kuuza au kutumia dawa zilizokwisha muda wa matumizi.
• Kukosa muda wa kuelekeza watumiaji wa dawa.
Sababu nyinginezo
• Kuutmia dawa za mifugo kwa binadamu.
• Kula bidhaa zinazotokana na wanyama (maziwa, nyama n.k) waliochinjwa muda mfupi baada ya kupewa dawa.
• Utupaji wa dawa kwenye mazingira yasiyosahihi.
Madhara ya usugu wa dawa.
• Kuongeza makali ya magonjwa.
• Husababisha vifo.
• Huongeza gharama za matibabu.
Nini kifanyike kudhibiti usugu wa dawa.
• Mgonjwa asitumie dawa kiholela.
• Mgonjwa asitumie dawa bila ushauri wa kitaalamu.
• Kuepuka kutumia dawa za mtu mwingine au kuchangia dawa.
• Mgonjwa ahakikishe anamaliza dawa alizopewa hata akipata nafuu.
• Mtoa dawa ahakikishe mgonjwa kaelewa matumizi ya dawa husika, atumie lugha inayoeleweka kiurahisi.
• Mgonjwa ahifadhi dawa vizuri.
• Kuepuka kuuza au kutoa dawa bandia au zilizokwisha muda wa matumizi yake.
Usugu wa dawa ni janga likuwalo kwa kasi duniani kote. Kutokana na utafiti inaonesha kua vimelea hutengeneza usugu dhidi ya tiba pendekezi (first line treatment).

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show