Ulaji wa Mpango

Kuna wengi ambao hula katika muda ambao mwili hauhitaji chakula chochote, katika muda usiopangiliwa. Ukiwa safarini, unaona karanga zinauzwa, unanunua na kutafuna. Baada ya muda, unafungua biskuti zako na juisi na kuendelea kula. Umemaliza, unafungua tena paketi za korosho na kuendelea kutafuna. Safari nzima tumbo linafanyishwa kazi bila kupumzika! Na cha kushangaza, unapofika mwisho wa safari, wakati wa usiku, unakula tena chakula kizito kisha kwenda kulala; bila kufahamu kuwa umelipa tumbo kazi inayoweza kuchukua hata usiku mzima! Unapoamka siku inayofuata, tumbo linapitishwa katika mchakato huohuo! Je, hii ni sahihi?

Tumbo lapaswa kupewa uangalizi makini. Halipaswi kufanyishwa kazi muda wote. Ni mojawapo ya viungo vya mwili vinavyotumiwa vibaya na kufanyishwa kazi kupita kiasi. Je, kiungo hiki hakistahili kupumzika? Baada ya kumaliza kazi yake baada ya mlo, usilipatie tumbo kazi nyingine tena kabla halijapata nafasi na muda wa kutosha wa kupumzika na kujipanga upya tayari kwa chakula kingine.

Baada ya mlo, tumbo lapaswa kupewa angalau masaa matano/sita bila kuongezewa chakula chochote. Katika muda huu, tumbo litamaliza kazi yake na kuwa tayari kupokea chakula kingine.

Pia, haipaswi kuwa na milo isiyo na muda maalum. Kama chakula kimeliwa saa moja au mbili kabla ya muda wake wa kawaida, tumbo linakuwa halipo tayari kufanya kazi yake kwa ukamilifu kwa kuwa bado halijakamilisha kumeng’enya na kusukuma mlo uliopita, na linakosa nguvu ya kuanza kazi mpya. Hivyo mfumo wa mwili unazidiwa.

Pia, si sahihi kuchelewesha chakula saa moja au mbili, kwasababu ya kazi au mazingira. Mfumo wa mwili umepangiliwa kwa namna ambayo mwili unajiandaa kupokea chakula katika muda maalum. Kama muda huu usipozingatiwa, mwili unapunguza ile nguvu na ari ya mfumo wa kumeng’enya na hivyo chakula hakishughulikiwi kama ipasavyo.

Tuanze kujenga tabia ya kula katika muda maalum kila siku, bila kuwahisha au kuahirisha muda wa kula, na bila kula chochote katikati ya milo. Mwili utafanya kazi kwa ufanisi zaidi pale unaposaidiwa! Anza sasa!

2 thoughts on “Ulaji wa Mpango

    1. Kuongezeka kwa appetite kunaweza kusababishwa na mambo mengi. Mwili ulivyoumbwa unaweza kujengeka kulingana na mazoea. Unapokula sana mara kwa mara unazoesha mwili kupokea kiwango hicho hivyo kisipofikiwa mwili utadai chakula kiongezwe. Pia baadhi ya magonjwa yaweza kuongeza hamu ya kula mf malaria, minyoo, nk

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show