Mlipuko wa Ugonjwa watokea Africa Kusini

Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) wamepata taarifa juu ya mlipuko wa ugonjwa uitwao listeriosis nchini afrika kusini, ambapo ugonjwa huu husemekana husambazwa kwa njia ya nyama.

Ila ugonjwa huu ni nini hasa?
Listeriosis ni ugonjwa unaosababishwa na aina ya bacteria aitwaye Listeria monocytogens.

Je, huyu bacteria anapatikana wapi ?

Huyu bacteria hupatikana kwenye mazingira yetu ya kawaida kama maji, kwenye udongo,kwa hiyo hii ina maanisha wanyama na mboga pia huweza vikaambukizwa muda wowote na mtu yeyote anaweza kuupata ugonjwa huu.

Bacteria huyu hupatikana sana kwenye vyakula au bidhaa zinazotokana wanyama kama ng’ombe au mbuzi. Bidhaa au vyakula kama:

 1. Maziwa yasiyocheshwa.
 2. Jibini( cheese)
 3. Nyama mbichi au soseji.
 4.  Mboga za majani na matunda.

Je, kundi gani la watu huweza kupata ugonjwa huu kwa urahisi?

 1. Watoto wachanga
 2. Mama wajawazito na watoto wao tumboni.
 3. Watu wenye magonjwa ya muda mrefu kama HIV, kisukari, ugonjwa wa saratani, magonjwa ya ini au figo.
 4. Watu wazee

Wanawake wajawazito huweza kupata ugonjwa kirahisi kwa sababu huwa kuna kuwa na upungufu wa kinga kiasi wakati mwanamke akiwa mjamzito.

Dalili za ugonjwa wa listeriosis.

Dalili huwa huweza kutokea kuanzia siku 3 hadi 70 baada ya maambukizi.

Kwa watu wenye afya ngangari, dalili ni kama;

 1. Homa
 2.  Kichefuchefu
 3. Kuharisha

Kwa kundi la watu kama wagonjwa wenye HIV, kisukari,mama wajawazito. Dalili ni kama:

 1. Dalili za ugonjwa wa uti wa mgongo au meningitis: mtu huwa na homa kali, hupata degedege, shingo kujikaza.
 2. kichwa kuuma sana na kwa nguvu, mtu huweza kuchanganyikiwa.

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu.

1.Hakikisha kwanza una mazingira safi nyumbani, vyakula kama nyama au maziwa vikae kwenye jokofu( freezer) ubaridi chini ya degree 4, matunda na mboga za majani kuoshwa kabla kuyatumia.

2.Nyama ichemshwe mpaka iive, maziwa yachemshwe vizuri.

3. Watu ambao huweza kupata ugonjwa huu kirahisi kama waathirika wa VVU, wenye kisukari au mama wajawazito waachane na kula au kutumia bidhaa zinazotokana na ng’ombe.Kama hamna maabukizi ya ugonjwa huu unaweza kutumia bidhaa.

 

1 thought on “Mlipuko wa Ugonjwa watokea Africa Kusini

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show