KUPASUKA KWA CHUPA YA UZAZI KABLA MIMBA KUTIMIZA WIKI 38

Chupa ya uzazi kwa kawaida huwa na maji ambayo husaidia kumlinda mtoto akiwa tumboni na husaidia katika kubadilishana kwa chakula na virutubisho vingine kati ya mama na mtoto, chupa hii hupasuka baaada ya wiki 38 au mwanzo wa uchungu wa kujifungua. Dalili yake huwa ni kutoka kwa maji katika uke wa mama mjamzito.
Chupa hii ya uzazi huweza kupasuka kabla ya wiki 38 na hali hii kitaalamu huitwa Premature rupture of membrane(PROM).
Hakuna sababu moja inayohusishwa katika kupasuka kwa chupa ya uzazi. Zipo sababu mbalimbali ambazo huchangia hali hii kutokea na huusisha;

•kutanuka zaidi kwa chupa ya uzazi kutokana na kuwa na maji mengi zaidi ya kawaida au mimba yenye watoto zaidi ya mmoja

• shingo ya uzazi kuwa dhaifu na kushindwa kushikilia mimba

• maambukizi kama vile UTI au maambukizi kwenye kuta za chupa ya uzazi

• Uvutaji wa sigara

• historia ya kupasuka kwa chupa ya uzazi katika mimba zilizopita au kutokwa damu wakati wa mimba.

Mara mama mjamzito aonapo dalili za kutoka maji ukeni inashauriwa apunguze shughuli na mizunguko. Inabidi apumzike na kuwahishwa kituo cha afya ili wataalamu wa afya wafanye vipimo na kuhakikisha kama ni chupa ya uzazi imepasuka. Matibabu mengine hutolewa kulingana na hali ya mama na mtoto.

 

Reviewed by Dr. Msiry

2 thoughts on “KUPASUKA KWA CHUPA YA UZAZI KABLA MIMBA KUTIMIZA WIKI 38

    1. Asante kwa swali lako.
      Ndio, mtoto wa wiki 30 anaweza akazaliwa na akawa mzima lakini atahitaji matunzo muhimu. Matunzo hayo humsaidia kukomaa vizuri kwani kwa kawaida mtoto hukomaa kuanzia wiki 38 kwenda juu.
      Hata hivyo mtoto njiti anakuwa katika hatari ya matatizo mengi ya kiafya katika kipindi hicho

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show