Athari za Kuchanganya Maziwa na Vyakula kabla ya Miezi Sita

 • Kwa miezi sita ya mwanzo maziwa ya mama ndio chakula cha pekee kwa mtoto.
 • Maziwa ya mama huwa na virutubisho vingi na chembechembe zinazo imarisha kinga ya mwili.
 • Mtoto anapozaliwa mfumo wake wa chakula unakuwa bado haujaimarika kikamilifu.Maziwa ya mama pekee ndiyo yanaweza kuimarisha mfumo huu.
 • Pale unapochanganya maziwa ya mama na vyakula vingine husababisha majeraha kwenye mfumo huu na kupelekea afya kuwa dhohofu na kushambuliwa na maradhi.
 • Pia mtoto anaweza kupata aleji na vyakula mbalimbali na kumnyima raha ya vyakula.
 • Mtoto akisha maliza miezi sita ndipo unaweza kumwanzishia vyakula vya nyongeza vilivyo katika mchanganyiko sahihi ukiendelea na maziwa ya mama mpaka mwaka mmoja.
 • Ili kupunguza maradhi ya mara kwa mara na makali ya maradhi mama zingatia kumnyonyesha mtoto kwa miezi sita ya mwanzo.

Mwanamke Jasiri haogopi Kunyonyesha.

12 thoughts on “Athari za Kuchanganya Maziwa na Vyakula kabla ya Miezi Sita

  1. Asante kwa swali Pius
   Maziwa yanapotunzwa kwenye chupa yanaweza ingia bacteria na kumdhuru mtoto.

   Pia virutubisho na chembechembe zinazoondoa sumu mwilini vinaweza haribika kutokana na kutohifadhiwa katika joto linalohitajika.

   Watafiti wa mambo ya saikolojia wanasema kumyonyesha mtoto hujenga uhusiano mzuri kati ya mama na mtoto na hili huweza changia kwenye tabia ya mtoto.

   Endelea kutumia daktari mkononi kwa mambo mazuri zaidi

  1. Asante kwa swali Pacilia
   Mama anae nyonyesha anashauriwa kula mlo ulio kamilika wenye matunda,vyakula asili ya nyama na nafaka.

   Ukiachana na hayo vitu kama vitunguu swaumu,mbegu za haladari (hupatikana masokoni) ,samaki wenye minofu myekundu nk husaidia kuongeza maziwa.

   Lamuhimu sana kuzingatia ni kunyonyesha ,kwani kitendo cha kunyonyesha husisimua mwili kutengeneza maziwa mengi zaidi.

   Endelea kutumia daktari mkononi kwa mambo mazuri zaidi.

 1. Helo.. Je unakuta mama amejifungua na maziwa hayatoki ama yanatoka kidogo sasa mtoto hashibi analia sana. Nashauriwa kumpa nini?

  1. Asante kwa swali Pendo
   -Maranyingi hii hutokea pale mama anapo jifungua kwa njia ya upasuaji.
   -Pia huweza kutokea kama mama anasumbuliwa na maradhi kama kisukari.
   -Au anapojifungua mtoto wake wa kwanza.
   Cha kuzingatia
   -Kujitahidi kunyonyesha hivyohivyo kwani kitendo cha kunyonyesha ndicho hufanya maziwa yaendelee kutengenezwa.
   -Kula mlo kamili, matunda yakutosha na ulaji wa vitunguu swaumu,mbegu za haladari na viazi vitamu vinasemekana kuongeza maziwa.
   -Pia tafiti zinasema mwili wa mama na mtoto ukugusana ngozi kwa ngozi wakati wa kunyonyesha husaidia.

   Kama tatizo halipungui muone daktari kwa uchunguzi zaidi.

 2. Habari

  Vipi kama mtoto kafikisha miezi minne na akataa maziwa ya mama. Bado atapata hizo athari kama akila vyakula vingne?

  1. Asante sana Brenda kwa swali.
   Kwa hali ya kawaida mtoto hatakiwi kukataa maziwa ya mama.
   Anaweza asipate au akapata madhara kutegemeana na mwili wake ulivyo jijenga.
   Miezi sita ni kiwango kinachoshauriwa kutokana na tafiti zilizo fanyika.
   Sababu zifuatazo zinaweza pelekea mtoto kukataa maziwa ya mama.
   -Mtoto anaweza kuwa na infection mwilini hivyo kupoteza hamu ya kunyonya.
   -Maziwa yanaweza kuwa yanatoka kwa kasi sana na kumfanya mtoto apate shida kunyonya.
   -Mtoto anaweza kuwa na vidonda mdomoni.
   -Mafuta au marashi ya mama yanaweza kumkera mtoto na kumfanya asitake kunyonya.
   -Uhusiano kati ya mtoto na mama kupungua kutokana na kutokuwa pamoja marakwamara.

   Itakapo tokea mtoto anakataa kunyonya gafla mama anaweza jaribu yafuatayo
   -Kumkamulia maziwa kwenye chupa au kikombe.
   -Kuacha/kupunguza matumizi ya chuchu za bandia (pacifier)
   -Kumyonyesha akiwa ametulia au akiwa na usingizi.
   -Kumsaidia kwa kuanza kubinya ziwa wakati anaanza kunyonya.

   Ikishindikana muone daktari kwa ushauri zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show