Uhusiano kati ya lishe na ugonjwa wa kifua kikuu

Hali ya lishe ya mtu huchangia kwa kiasi kikubwa uwezo wa mwili kupambana na maambukizi mbalimbali. Hali duni ya lishe huweza kusababisha kupungua kwa kinga ya mwili na hivyo kuongeza uwezekano wa mtu kupata maradhi ikiwemo kifua kikuu

Athari za ugonjwa wa kifua kikuu kwenye lishe
Vimelea vya kifua kikuu vinapoanza kuzaliana mwilini, mahitaji ya virutubishi huongezeka na hivyo huweza kusababisha uzito wa mwili kupungua hata kabla ya mtu kugundua kama ana ugonjwa wa kifua kikuu. Wakati huo huo, dalili zinazojitokeza kwa mgonjwa wa kifua kikuu kama vile kukosa hamu ya kula, kutapika, homa na kukohoa huchangia mtu huyu kushindwa kukidhi ongezeko la mahitaji ya virutubishi mwilini.
Vilevile, kutokana na mabadiliko yanayotokea mwilini, ufanisi wa matumizi ya virutubishi kama vile protini huweza kupungua. Ulaji duni, ongezeko la mahitaji ya virutubishi na kupungua kwa ufanisi wa utumikaji wa virutubishi huweza kusababisha utapiamlo

Athari za lishe duni kwenye kifua kikuu

Mtu mwenye utapiamlo yupo katika hatari zaidi ya kupata uambukizo wa kifua kikuu kwani kinga yake ya mwili ni dhaifu. Endapo mtu alipata uambukizo ule ambao haonyeshi dalili, wakati hali yake ya lishe na afya ni thabiti, akipata utapiamlo vimelea hivyo huanza kuzaliana na hivyo huweza kusababisha kuugua kifua kikuu.
Utapiamlo kwa mgonjwa wa kifua kikuu husababisha kurefusha kipindi cha kuugua, mwili hudhoofika zaidi, kushindwa kukabiliana na matatizo ya kiafya yanayoambatana na ugonjwa wa kifua kikuu na pia ufanisi wa matibabu huweza kupungua.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show