Maambukizi ya sikio la Kati kwa watoto(Otitis Media)

Maambukizi ya sikio la kati (Middle Ear) ni kati ya magonjwa mawili ya juu yanayosumbua sana watoto baada ya magonjwa ya Mfumo wa juu wa upumuaji (URTI)

Kulingana na maumbile ya mrija (Eustachian tube) unaounganisha mifumo hii miwili husababisha watoto kupata maambukizi ya maskio kirahisi kuliko watu wazima

Asilimia 90 ya watoto hupata maambukizi haya angalau mara moja kabla hawajavuka miaka mitano

Vitu vinavyopelekea kupata maambukizi ya sikio
1)Umri wa mtoto.maambukizi haya huwapata sana watoto chini ya miaka mitano sanasana
2)Mafua yasiyoisha,husababisha kuziba kwa mrija wa Eustachian na kusababisha kujaa kwa sikio la kati(Middle ear) hivyo kuongeza uwezekano wa wadudu kujaa na kuleta maambukizi ya sikio
3)Kunyonyesha kwa chupa
4)Mlundikano wa watoto mfano.Shule za awali huongeza maambukizi kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine
5)Watoto wenye magonjwa ya kuzaliwa mfano.Downs syndrome,Ukimwi ,kisukari

Dalili zake ni zipi?
1)Maumivu ya maskio
2)Kupungua kwa usikivu wa mtoto,mzazi anaweza kuona mtoto anasikia mpaka upaze sauti kidogo,anakasirika kirahisi
3)Kizunguzungu na maumivu ya kichwa
4)Mtoto anaweza kuwa na homa na hata kupunguza hamu ya kula
5)Majimaji kutoka kwenye maskio,hii ni hatua ya baadae kabisa kama mtoto atakuwa na maambukizi makali au yanayojirudia bila kupona

Jinsi ya kujikinga
1)Usafi kitu cha muhimu kuzingatia
2)Kupunguza matumizi ya chupa kwa ajili ya kunyonyesha
3)Epuka vitu vinavyomletea mwanao madhara ya allergy mf.vumbi,baadhi ya vyakula

Nini cha kufanya
1)Kuwahi kituo cha afya.daktari atafanya uchunguzi wa maskio,mdomo na pua kuangalia dalili zozote zinazoweza kuleta shida kwenye maskio
2)Bakteria ndio wanaongoza kusababisha maambukizi haya hivyo antibiotics hufanya kazi vizuri
3)Dawa za kupunguza maumivu n.k

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show