Je, ninaruhusiwa kunywa kahawa?

Kahawa ni kinywaji ambacho wengi wanakipenda kutokana na sifa yake ya kuamsha akili na kuondoa usingizi. Kahawa inakemikali iitwayo caffeine ambayo ndio inasababisha hali hiyo. Kemikali hii pia inapatikana katika vinywaji kama baadhi ya soda na vinywaji vya kuongeza nguvu kama vile redbull na azam energy drink. Swala la mgonjwa wa moyo kuruhusiwa kunywa kahawa au laa linategemea sana jinsi caffeine inavyo muathiri mgonjwa mwenyew. Caffeine inaweza sababisha ongezeko la shinikizo la damu na mapigo ya mayo.

Kwa watumiaji wa muda mrefu hali inaweza isiwepo ila hata hivyo wanashauriwa kutozidisha vikombe viwili vidogo vya kahawa kwa siku.

Kwa wale wanaotumia kahawa kwa mara ya kwanza au ambao sio watumiaji wa mara kwa mara kahawa inaweza kuongeza shinikizo lao la damu kwa kiasi cha 13/7mmHg kutoka kiasi cha kawaida. Kwa mtu huyu inashauriwa kutumia kahawa isiyo na caffeine (decaffeinated coffee) kama mbadala.

Wachache wanalazimika kuacha kabisa kunywa kahawa na vinywaji vingine vyenye caffeine kutokana na kupata athari kubwa zaidi kuliko wengine. Hawa wanashauriwa kupunguza kiasi cha kahawa walichokuwa wanakunywa taratibu siku hadi siku mpaka pale watakapo acha ili kuzuia hali ya kichwa kuuma kutokana na kuacha ghafla.

Kwa ujumla haishauriwi kunywa kahawa kabla ya shughuli yoyote inayoweza kuongeza shinikizo la damu na mdudo wa moyo kama vile kufanya mazoezi.

Athari hizi huonekana hasa kwa watu ambao tayari wanamagonjwa ya moyo. Kwa ambao sio wagonjwa wa moyo tafiti zinaonyesha kuwa unywaji wa kahawa hausababishi magonjwa ya moyo na huweza kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.

1 thought on “Je, ninaruhusiwa kunywa kahawa?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show