Huduma ya kwanza kwa aliyeteguka mguu.

Kuteguka mguu kitaalamu sprain ankle ni hali inayotokana na ligamenti(Kano) kukatika kidogo au moja kwa moja kutokana na ajali.

Kuteguka mguu hutokea mara kwa mara hasa katika maungio ya unyayo ya mguu, na husababishwa na presha kubwa inayowekwa katika mguu kwa haraka mfano kwa wachezaji wa mpira au wakimbiaji.

Dalili za kuteguka mguu
Maumivu makali sana.

-Kuvimba kwa haraka sehemu iliyoteguka.

Huduma ya kwanza kwa aliyeteguka.

Upumzishe mguu ulioteguka japo unaweza ukakanyagia au kuutembelea hii inategemea na kiasi cha maumivu.

Kanda eneo lenye uvimbe kwa kitambaa chenye maji baridi au kwa kutumia barafu kwa muda mchache.

Weka mguu juu ya mito wakati wa kulala ili kupunguza uvimbe.

Funga mguu kwa bandeji hasa eneo lenye uvimbe na usikaze sana bandeji.

Mara nyingi kuteguka kunakuwa hakuna madhara makubwa na unaweza jipatia huduma ya kwanza mwenyewe

Fika katika kituo cha afya kama una dalili zifuatazo:

○Huwezi kabisa kuutumia mguu

○Maumivu makali kutoka kwenye mfupa.

○Rangi ya ngozi ya sehemu ya uvimbe kubadilika.

“Kumbuka kuteguka mguu kunaweza pelekea kutopona kama hutozingatia matibabu”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show