Hatua kuu 4 za maambukizi ya Kaswende

Hadithi moja ya zamani ninayoikumbuka ambayo walikuwa wakiadithia nanukuu “huwezi pata magonjwa ya zinaa kama kaswende kama ukijiosha vizuri na kwenda chooni kupata haja ndogo baada ya kujamiana bila kinga”.

Hizi zote ni hadithi ila sio ya sasa kwani utafiti wa mwaka 2011 umebaini kuwa kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Kaswende asilimia 2.5 ya kina mama wajawazito waliohudhuria kliniki wamegundulika wameambukizwa.

 

Kaswende ni ugonjwa hatari wa kuambukizwa unaosababishwa na bakteria anayefahamika kwa jina la T.pallidum

Njia za maambukizi

a)kwa kujamiiana na aliyekwisha ambukizwa

b)kwa kuongezewa damu yenye maambukizi

c)kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto


Najuaje nina Kaswende?

Kaswende hutokea katika hatua kuu 4 katika muda tofauti tofauti.

●Hatua ya kwanza:Ni hatua inayotokea siku 10 hadi miezi mitatu baada ya maambukizi ambapo aliyeambukizwa hutokewa na vidonda vidogo vidogo visivyo na maumivu maeneo ya sehemu za siri, mdomo,mikononi na kwingineko.Japo hupona vyenyewe.

Hatua ya pili:Hii huanza wiki 2 hadi 10 baada ya hatua ya kwanza kutokea na huambatana na kutoka kwa vipele vidogo vidogo kama vya joto na ambavyo hupona bila matibabu pamoja na dalili kama homa, kupungua uzito, maumivu ya kichwa na nyinginezo.

Hatua ya tatu:Hii ni hatua ambayo mgonjwa haonyeshi dalili zozote.

Hatua ya nne:Hii ni hatua mbaya ambayo kama mgonjwa hakugundulika na kutibiwa mapema husababisha madhara makubwa mwilini hasa kwenye ubongo, moyo na mishipa ya damu ambapo hupelekea kusababisha kupoteza kumbukumbu, kuwa kipofu na pengine kifo.

“Matumizi sahihi ya kondomu imechangia kwa asilimia kubwa katika kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama Kaswende, vyema ukatumia kuepuka maambukizi”

 

2 thoughts on “Hatua kuu 4 za maambukizi ya Kaswende

 1. Asante dokta kwa maelezo,je mtoto akiambukizwa kaswende kutoka kwa mama anakuwaje…yani anaonesha dalili zipi?!

  1. Shukrani kwa swali na karibu daktari mkononi.
   Mtoto akiambukizwa ugonjwa wa kaswende huonesha dalili kama hizi
   Homa
   Vipele vidogo vidogo kama vya joto
   Anashindwa kukua vizuri
   Kuwa na mapungufu katika baadhi ya viungo kama pua na meno
   Matatizo ya kusikia na kuona
   Hizi dalili zinaweza zisitokee zote ila ni kati ya dalili ambazo anaweza kuwa nazo.
   Shukrani tena kwa swali na kama bado hujaridhika na majibu unaweza uliza.
   Karibu daktari mkononi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show