Fahamu vyanzo na dalili za vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo ni vidonda vya mfumo wa umeng’anyaji chakula vinavyotokea baada ya kuta /leya za tumbo kuchubuka au kuharibika..

Vidonda hivi vikitokea tumboni tunaviita “Gastric ulcer” na vikitokea katika utumbo mara tu baada ya tumbo tunaviita “Duodenal ulcer”

Nini vyanzo vya vidonda vya tumbo
Vidonda vya tumbo husababisha na asidi kuongezeka kupita kiasi na kufanya uharibifu wa kuta za tumbo kiasi ata vilinda ukuta vinashindwa zuia… Asidi hii inaweza ikawa kutoka katika vyakula tunavyokula au asidi asilia iliopo tumbonhi ikiongezeka

Zifuatazo ni vyakula vinavyoongeza asidi mwilini
1. Vyakula vyenye kaffein
2. Pilipili
3. Matunda machachu
4. Pombe kali

Zifuatazo ni sababu zinazofanya asidi izalishwe kwa wingi tumboni
1. Mawazo au mafhadhaiko yaliyopita kiasi
2. Hasira
3. Vyakula vyenye viungo vingi

Nini dalili za ugonjwa huu
1.maumivu makali sehemu ya mwili yenye vidonda hivyo
2. Kiungulia
3. Tumbo kujaa gesi
4. Tumbo kuwaka moto
5. Kukosa choo au kupata choo kwa shida
6. Kukosa hamu ya kula au kula kupita kiasi
7. Kichefuchefu
8. Kizunguzungu
9. Kukosa usingizi
10. Maumivu ya mgongo au kiuno

Hivyo ni vyakula gani vinafaa kwa watu wenye vidonda vya tumbo?
1. Kabeji
2. Asali
3. Ndizi
4. Uwatu
5. Vitunguu swaumu
6. Unga wa majani ya mlonge

6 thoughts on “Fahamu vyanzo na dalili za vidonda vya tumbo

  1. Maziwa yana asidi kiasi kitu ambacho hufanya yasiwe salama kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo.. ila huweza saidia kidogo mwanzoni unapokunywa maana huziba kuta za tumbo na kufanya maumivu ya tulie kwa muda kidogo ila baadae huisha na kusababisha asidi nyingi zaidi izaliwe hivyo kunywa kwa kiasi angalau glasi moja kwa siku kwasababu ukizidisha huleta madhara na sio tiba.

 1. Doctor katika dalili hizo tajwa mm ni kichefu chefu ambacho huja mara chAche hasa nikinywa juice ya mua au tende au mara nyingine maji nikiwa na kiu sana je hiyo pia ni dalili ya vidonda vya tumbo

  1. Asante kwa swali…
   Kichefuchefu hicho huja ukiwa na kiu au baada ya kunywa hivyo vinywaji?

   Kama ni baada inaweza kuwa tu ni hivyo vinywaji lakini kama ni kabla hujnaywa chochote inaeza ikawa ni dalili lakini kwa vidonda vya tumbo kichefuchefu hueza tokea muda wowote ila hasa ukiwa na njaa.. ningependa ujaribu kuangalia na dalili zengine kama unazo ili urizike zaidi…

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show