Kung’ata kucha; nifanye nini ili niache tabia hii!?

Karibia nusu ya watoto wote na vijana huwa na tabia ya kung’ata kucha zao. Kuna baadhi ambao hukua na kuendelea na tabia hiyo mpaka wanavokua watu wazima kwa sababu tu walishindwa kuacha wakiwa watoto.

Wanasayansi hawana uhakika kama jambo hili ni la kurithishwa lakini kwa tafiti mbalimbali zilizofanyika inaonesha kwamba wazazi wengi waliokua waking’ata kucha wana uwezekano mkubwa wa kupata watoto watakaokuwa na tabia hii. Hujitokeza pia hata kama mzazi aliacha kung’ata kucha kabla mtoto wake hajazaliwa.

Kwanini watu huendeleza hali hii!?
Huweza kujitokeza endapo mtu ana;

 • Msongo wa mawazo.
 • Hasira, woga au kuwa na huzuni.
 • Njaa.
 • Kukosa kujiamini au kuudhika.

“Kung’ata kucha huwa ni njia anayoitumia mtu kukabiliana na hisia hizo.

Kwanini uache kung’ata kucha!?

 1. Hufanya kucha zako kuwa na muonekano mbaya; hii hutokana na kuharibika kwa tishu zinazozunguka kucha na hivyo kuingilia mfumo mzuri wa ukuaji wa kucha zako.
 2. Huweza kuharibu tabasamu lako; kuna uwezekano wa wewe kuchubua au kuvunja meno yako wakati unang’ata kucha. Hali ikiendelea zaidi inaweza kusababisha matatizo kwenye taya.
 3. Huweza kukuletea magonjwa; mikono ni sehemu inayotunza vimelea vya magonjwa vya aina mbalimbali. Unapoweka vidole mdomoni unaongeza uwezekano wa kuingiza vimelea hivi katika mwili wako. Uharibifu wa ngozi pia wakati wa kung’ata kucha unatengeneza mazingira mazuri ya vijidudu kupenya.

Jinsi ya kuepuka hali hii.
Unaweza kujaribu njia zifuatazo;

 • Kata kucha zako na kuziacha fupi kila wakati; hii itasaidia kutong’ata kucha zako maana ufupi wake hautakuridhisha kuzing’ata.
 • Zipake rangi; tumia rangi zenye ladha kali ambayo itakupelekea ujiulize mara mbili pale unapotaka kuzitafuna.
 • Vaa gloves; hii inafanya kazi kwamba huwezi kung’ata kucha usizoziona. Endapo ratiba yako ya kila siku haitakuruhusu kuvaa gloves unaweza kubandika stika maalum kwa ajili ya kuziba kucha.
 • Tafuta kisababishi chako; jaribu kujichunguza kwamba ni hali gani hasa huwa inakupelekea wewe kung’ata kucha na ukishaipata jaribu kutafuta njia nyingine ya kukabiliana na hali hiyo.
 • Ushughulishe mdomo wako; jaribu kuwa na kitu mdomoni mara kwa mara kama kutafuna banzoka (chewing gum). Hii itaupa mdomo wako kazi nyingine zaidi ya ile ya kung’ata kucha.

Jambo la kuacha kung’ata kucha siyo la usiku mmoja; huhitaji muda, bidii na malengo. Ukishindwa njia hizo hapo juu unaweza kujiwekea utaratibu wa kuacha kucha moja baada ya nyingine mpaka utakapofanikiwa.

7 thoughts on “Kung’ata kucha; nifanye nini ili niache tabia hii!?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show