Madhara ya homa ya matumbo na jinsi ya kuepuka (typhoid)

Madhara yatokanayo na homa ya matumbo (typhoid fever).

Homa ya matumbo isipo tibiwa kwa wakati inaweza kukuletea madhara yafuatayo mwilini;

1. Kuvuja damu kwa ndani kwenye mfumo wa chakula.

Hii ni kwasababu bakteria (vijidudu) vinavyo sababisha ugonjwa huu vinaharibu kuta za mfumo wa chakula kwa kuzishambulia na kufanya ziharibike na kuvuja damu. Dalili zifuatazo huonekana kwa mtu ambaye anavuja damu kwa ndani kwenye mfumo wa chakula.

a. kusikia uchovu sana
b. kukosa pumzi afanyapo shughuli ndogo
c. ngozi kupauka na viganja kuoneka vyeupe kuliko kawaida
d. mapigo ya moyo kwenda mbio
e. kutapika damu

f.  kutoa haja kubwa yenye rangi nyeusi au yenye dam

2. Kutoboka kwa kuta za mfumo wa chakula.

Hii sasa sio tu kutoka damu bali nikutoboka kabisa na kusababisha hawa bakteria wanao sababisha homa ya matumbo kusambaa sehemu zingine za mwili na kuleta shida katika mwili wote.

Jinsi ya kujikinga na homa ya matumbo.

1. Kunawa mikono kwa kutumia maji safi na sabuni.
Kabla ya kula kitu chochote na baada ya kutoka chooni/msalani

2. Epuka kunywa maji yasiyo salama.
Maji ambayo hayajachemshwa, kuchujwa na kuhifadhiwa katika vyombo visafi, au maji ambayo hayaja wekwa waterguard si salama kwa kunywa.

3. Epuka kula chakula ambacho maandalizi yake hayapo katika hali ya usafi au kuhifadhiwa katika vyombo visafi.

4. Epuka kula matunda bila kuoshwa vizuri au bila kumenywa kama inavyo takiwa
Mfano: watu hupenda kula embe bila kumenya maganda, basi hakikisha limeoshwa kwa maji safi ya uvuguvugu.

5. Epuka kunywa juice ovyo mtaani hasa za matunda zinazotengenezwa majumbani.
Hii ni kwasababu huna uhakika na maji yaliyo tumika kutengeneza vinywaji hivi kama ni safi na salama. Pia ni vyema watengenezaji kuzingatia hili.

6. Beba sanitizer mkono hii itasaidia endapo mahali ulipo hakuna maji ya kunawa, unahitaji kushika chakula na hakuna njia yeyote mbadala.

Muhimu zaidi ni usafi kiujumla wa mazingira, maji na chakula. Tuwalinde watoto kwa kuwanawisha na kuwahimiza kuzingatia usafi pia ili kuepukana na homa ya matumbo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show