Jinsi ya kutibu tatizo la jicho kua jekundu(red eye).

Matumizi ya dawa kutatua tatizo hili hutofautiana kulingana na sababu zilizopelekea jicho kuwa jekundu(red eye).

Huweza kuwa dawa kwa ajili ya virusi, dawa za kupunguza uvimbe na maumivu, dawa zizuiazo koligen (anti-cholinergics) dawa ziwezeshazo mtu kupunguza kiasi cha maji kwenye jicho (diuretics).

 • Dawa za kupaka kwa ajili ya virusi (topical anti-viral).
  Dawa kama trifluridine, ganciclovir, acyclovir, husaidia kwa jicho ambalo litakua limeathiriwa na vimelea aina ya virusi. Huharibu DNA ya virusi na kuwaua.

 

 • Dawa za kupunguza maumivu na uvimbe (NSAIDs).
  Dawa hizi husaidia kupunguza kiasi cha damu kiingiacho kwenye jicho hivo kupunguza maumivu na wekundu wa jicho. Haipunguzi presha iliyokua imetawala jicho. Hupunguza maumivu mara moja na hupunguza tatizo la kuogopa mwanga (photophobia). Dawa hizo ni kama; diclofenac ya kupakaa, ketorolac tromethamine al maarufu Acular/ Acuvail, flurbiprofen nk.

 

 • Dawa zizuiazo koligen (anticholinergics).
  Dawa hizi husaidia wenye matatizo ya ‘glaucoma’ (presha ya macho). Hufanya mishipa ya damu ya jicho kupunguza kiwango chake cha kupitisha damu kwa kupunguza njia yake. Watu wengine hupata tatizo la kuumwa paji la uso siku chache baada ya kuanza matumzi ya dawa. Dawa hizo ni kama; pilocarpine au pilopine HS.

 

 • Dawa za kupunguza maji kwenye jicho.
  Dawa hizi hupunguza kiasi cha maji kilichojikusanya kwenye jicho na kupunguza presha iliyopo katika jicho. Mfano; mannitol (osmitrol).

 

 • Dawa za kulainisha jicho (lubricants).
  Hizi hulainisha na kupunguza msuguano kati ya jicho na kuta za jicho hivo huzuia jicho kuuma na kuendelea kuvimba. Hufanya kazi ya machozi (kuongeza maji kwenye jicho). Husaidia pia watu wenye macho makavu. Dawa hizi ni; artificial tears (machozi ya bandia), genteal, isopto tears nk.

 

 • Antihistamines.
  Hizi ni dawa za aleji. Ambazo hutumika hapa ni zile zilizotengenezwa maalum kwa ajili ya jicho. Hutibu matatizo ya jicho kuwasha ambayo husababisha jicho kuvimba na kuuma pale tunapoyakuna. Dawa hizi ni kama; olopatadine, ketotifen (Zyrtec itchy eye).

 

 • Antibayotiki.
  Vimelea aina ya bakteria huweza kusababisha jicho kua jekundu hivyo matumizi ya antibayotiki huweza kuhitajika pale tu itakapo thibitishwa na mtaalamu wa macho kua ni vimelea vya bakteria. Dawa hizi ni; ofloxacin ya macho, ciprofloxacin ya macho. Moxifloxacin ya macho, erythromycin ya macho, bleph 10, gentamycin nk.

Hizo ni baadhi tu ya dawa ambazo hutumika katika matibabu ya uwekundu wa macho.

 “Inashauriwa kufika kituo cha afya kupata matibabu kwani unywaji wa madawa holela unamadhara”

2 thoughts on “Jinsi ya kutibu tatizo la jicho kua jekundu(red eye).

 1. nina ndugu yangu anashida ya macho, aligundulika kuwa mishipa inayopeleka damu kwenye macho imeziba hivo uonaji wake ni hafifu, alipewa dawa ila bado haoni vizuri

  1. Shukrani kwa swali na karibu daktari mkononi.
   Ni vyema akamuona daktari aliyempa dawa mara ya kwanza ili aendelee kumtibu ila kama anaonatatizo linazidi kuwa baya ni vyema akamuona daktari bingwa wa macho eneo alipo.
   Shukrani na endelea kututembelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show