Njia asili za kutibu fangasi za ukeni

Je, wajuaa jinsi ya kutatua tatizo la fangasi ukeni?

tujikumbushie kidogo fangasi ni nini.

Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Leo hatutaongelea sana juu ya nini husababisha hizi fangasi sehemu ya uke. Kujua hili tembelea tovuti ya  https://daktarimkononi.com/2018/03/03/tatizo-la-fangasi-ukeni-limekua-ni-la-kudumu-kwangu/. Leo tutaongelea njia asili za kutibu fangasi za ukeni. Njia hizo ni kama:

JUISI YA MALIMAO (Lemonade):

Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo. Kunywa robo lita (ml 250) kutwa mara 2 kwa siku 10 kwa mtu mzima na glasi ndogo moja kwa siku kwa mtoto wa miaka miwili mpaka kumi. Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea ladha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii kila unpotoka kula chakula cha mchana  au cha jioni.

MAZIWA YA MTINDI:

Mtindi au bidhaa zitokanazo na maziwa ya mtindi ni tiba ya kuaminika ya fangasi wa ukeni. Pia inashauriwa kula tuu huu mtindi kiasi cha kutosha kila siku.

KITUNGUU SWAUMU:

Kitunguu swaumu kina sifa na uwezo wa kuua bakteria na hata virusi mwilini. Vikatekate (chop) vipande vidogo. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya  kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

MAFUTA YA NAZI:

Kama fangasi hao wa ukeni wanajitokeza hadi sehemu kidogo ya nje ya uke na unapata muwasho pia, hakikisha unapakaa mafuta ya asili ya nazi yaliyotengenezwa nyumbani. Hii dawa tosha kwa fangasi wowote juu ya ngozi.

MAMBO MHIMU YA KUZINGATIA:

Fangasi hii inaweza ikachelewa kupona au ikawa inajirudia hata baada ya kupona kwa sababu zifuatazo:

  • Kutokunywa maji ya kutosha. (glasi nane kwa siku kwa mtu mzima).
  • Matumizi ya vyakula vyenye wanga kwa sana.
  • Matumizi ya sukari kwa sana. (hushauriwa kutumia asali).
  • Matumizi ya vinywaji vya baridi, chai, kahawa.
  • Matumizi ya pafyumu na kuweka vitu nani ya uke.
  • Matumizi ya vidonge via uzazi wa mpango. Huweza kutumia njia mbadala za kujikinga na mimba.
  • Epuka kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

2 thoughts on “Njia asili za kutibu fangasi za ukeni

    1. Habari yako Vanny. Tunashukuru kwa kuendelea kufurahia kazi yetu. Kwa kujibu swali lako, ndio uke ni sehemu nyeti sana na husahuriwa kutokusumbuliwa kwa kuwekwa vitu visivyo husika. Njia hizi za kujitibu na fangasi ni za kumeza na kunywa na sio kwa kuweka vitu hivo katika sehemu ya uke hivo havitaingiliana na usafishaji wake wa moja kwa moja. Endelea kufurahia na kutumia huduma zetu za daktari mkononi. Pia usisahau kuwasiliana nasi kwa kutumia namba 0688636717 au 0762952137 😊.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show