je, wajua njia za kuzuia mimba endapo umejamiiana bila kinga?

je, wajua njia za kuzuia mimba endapo umejamiiana bila kinga?

Mara nyingi ajali hutokea. Ndio sababu ya kuwepo kwa uzazi wa mpango wa dharura (emergency contraception) ambao ni njia salama na yenye ufanisi kuzuia mimba hadi siku 5 baada ya ngono isiyozuiliwa.

Uzazi wa mpango wa dharura ni njia salama ya kuzuia mimba baada ya kujamiiana bila kinga. Kuna aina chache za  njia ya kuzuia mimba kwa dharura, na baadhi kuwa bora kuliko nyingine.

Kuna njia ngapi za dharura za kuzuia mimba?

njia ya 1: Kuwekewa kitanzi  ndani ya saa 120 (siku 5) baada ya kujamiiana bila kujikinga. Hii ni njia bora zaidi  kuzuia ujauzito.

njia ya 2: Kutumia vidonge vya kuzuia mimba ya dharura (morning-after pills) ndani ya saa 120 (siku 5) baada ya kujamiiana bila kujikinga.

morning-after-pill
A box of Microgynon contraceptive pills, produced by Bayer AG, sits on a pharmacy counter in this arranged photograph in London, U.K., on Monday, Dec. 14, 2015. European pharmaceuticals stocks in 2015 have outperformed the Stoxx 600 Index by 1.2 percentage points in U.S. dollar terms. Photographer: Simon Dawson/Bloomberg via Getty Images
xshutterstock_135468857-750x375.jpg.pagespeed.ic.hJY9H9U8Y5

Microgynon 30 ni moja ya kidonge maalumu cha kuzuia mimba. kati ya vingi ambavo hutumika kama ‘morning-after pills’. Microgynon 30 ina aina mbili za homoni, estrogen na progestin, ambayo ni kawaida kupatikana kwenye vidonge vya uzazi wa mpango. Kidonge hiki kinaweza kuwa na ufanisi hadi 99% katika kuzuia mimba. Katika matumizi ni vema kupata ushauri wa daktari  au nesi pale dharura itakapojitokeza.

chanzo kinachoweza pelekea matumizi ya vidonge vya
dharura vya kuzuia ujauzito (morning-after pills) ni;

  •  Kutotumia kondomu au mbinu zingine kama njia za uzazi wa mpango.
  • Kutotumia dawa za uzazi wa mpango kwa majira kama ulivyo shauriwa na daktari au kubadili kitanzi.
  • Kondomu  kupasuka baada ya kumwaga shahawa.
  • Mwenza wako kuchelewa kujitoa kabla ya kumwaga shahawa katika kujamiiana.
  • kulazimishwa kufanya mapenzi au kubakwa.

vidonge vya dharura vya kuzuia ujauzito hufanya kazi vipi?

Ujauzito hautokei tu mara baada ya kujamiiana, ndio maana inawezekana kuzuia mimba siku chache baada ya wewe kufanya hivyo. Hasa  kuwahi mapema kutakapozingatiwa. Mbegu za kiume huishi ndani ya mwili wa mwanamke  hadi siku 6 baada ya ngono, kusubiri yai kuonyesha. Kama ovulesheni ikitokea wakati huo, mbegu za kiume inaweza kukutana na mayai na kusababisha mimba.  Vidonge vya dharura za kuzuia ujauzito hufanya kazi ya kukomesha ovari kutoa yai kwa muda. Vilevile vidonge hivi haviwezi fanya kazi kama ovulesheni imekwisha tokea.

“matumizi ya ‘morning-after pills’ huniondolea hofu ya kuwa mjamzito, wewe je?”

Matumizi sahihi ya vidonge  vya dharura kwa baada ya kujamiiana, inasaidia kuwepo na uwezekano mdogo sana wa kupata ujauzito. Lakini usitumie njia ya dharura mara kwa mara kama ulinzi wako pekee kuepukana  kupata ujauzito, kwa sababu sio ya ufanisi, ukilinganisha na mbinu za kudhibiti ujauzito zisizo za dharura (kama matumizi ya kitanzi, vidonge cha uzazi wa mpango, au kondomu).

kwa maswali yoyote usisite kuuliza kwa msaada zaidi.

9 thoughts on “je, wajua njia za kuzuia mimba endapo umejamiiana bila kinga?

  1. Thanks very much for such education. With this online learning learning platform we can serve majority of people who are unaware of different health disorders.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show