Fahamu kuhusu homa ya ini aina A (hepatitis A)

Kuna aina tatu za homa ya ini (Hepatitis), A B na C. Homa ya ini aina A inasababishwa na maambukizi ya kirusi kupitia haja kubwa kutoka kwa mtu aliye na haya maambukizi.
Inapatikana sehemu ambazo kuna mazingira machafu, wanaume wanaojamiiana na wanaojichoma sindano za madawa ya kulevya.
Homa ya ini aina A mara kwa mara hukaa kwa miezi mingi na ni nadra sana, pia sio hatarishi kama homa ya ini aina nyingine (aina B) na watu hupona kabisa ndani ya miezi kadhaa. Kwa watoto, dalili zinaweza zisioneshe kabisa.
Kuna chanjo inaptikana kwa ajili ya watu walio na uhatarishi mkubwa wa kuupata.

DALILI ZA HOMA YA INI AINA A;
Dalili hua zinaanza kujitokeza ndani ya wiki nne(4) baada ya kupata haya maambukizi, ingawa sio kila mtu ataonyesha dalili zote.
Baadhi ya dalili ni kama;
• Maumivu ya mifupa na misuli
• Mwili kuchoka choka na kuumwa
• Homa
• Kukosa hamu ya chakula
• Maumivu kwenye tumbo la juu
• Manjano ya macho au ngozi
• Muwasho wa ngozi
• Mkojo giza na kinyesi rangi

MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI AIAN A.
Mtu mwenye homa ya ini anaweza kusababisha maambukizi wiki mbili kabla ya kuanza kuonyesha dalili hadi wiki baada ya kuonyesha hizo dalili
Unaweza pata maambukizi ya manjano kupitia;
• Kula chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye maambukizi ambaye hajanawa mikono vizuri au kanawa na maji yenye hao virusi
• Kunywa maji yaliochafuliwa na virusi vya homa ya ini
• Kula chakula kibichi au ambacho hakijapikwa vizuri
• Kujamiiana na mtu mwenye haya maambukizi
Watu walio na hatari ya kupata haya maambukizi wanashauriwa kuchoma chanjo ili kupunguza uwezekano wa kupata huu ugonjwa

TIBA YA HOMA YA INI AINA A.
Homa ya ini aina A haina tiba, ila huwa inapona yenyewe ndani ya miezi kadhaa.
Unashauriwa kumuona daktari kwa ajili ya kupima damu kama unahisi una haya maambukizi, hasa dalili zikizidi kuwa mbaya, kwasababu kunaweza kuwa na uwezekano wa kuwa na magonjwa makubwa mengine. Daktari anaweza akakushauri dawa za kutumia na pia kuchukua vipimo kadhaa kuhakikisha kama ini lako linafanya kazi vizuri.

Chanjo za Homa ya ini aina A;
Kuna aina tatu za chanjo ya hepatitisi A;
– Chanjo ya hepatitisi A peke yake
– Chanjo muunganiko ya hepatitisi A na B
– Chanjo muunganiko ya hepatitisi A na matumbo (typhoid)
Ongea na daktari wako aweze kukushauri ipi ni bora zaidi kwa hali yako. Kama unasafiri kwenda nje, inashauriwa kuchoma wiki mbili au tatu kabla ya kusafiri hata pia iyo siku unayosafiri. Dozi za ziada zinashauriwa miezi 6-12 kama unahitaji ulinzi wa muda mrefu.

USHAURI UFUATAO UNAWEZA UKASAIDIA;
• Pumzika vya kutosha hasa kipindi cha awali cha dalili
• Tumia dawa za maumivu kama paracetamol au ibuprofen
• Punguza muwasho kwa kukaa kwenye mazingira masafi na hewa nzuri
• Kula chakula kidogo au vyakula vyepesi kuzuia kutapika ama kichefuchefu
• Usitumie pombe ya aina yeyote ili kuzuia madhara yoyote zaidi kwenye ini.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show