Ujue ugonjwa wa mshipa wa ngiri (hernia) na matibabu yake.

Ngiri ni uvimbe unaotokana na viungo vya ndani ya mwili kusukuma kuta za misuli inayozunguka au kushikilia viungo hivyo na kuviweka mahala pake.Ngiri hutokea pale ambapo kuna udhaifu au uwazi katika kuta za misuli na hivyo kuruhusu viungo vya tumbo kupenyeza na kujenga uvimbe upande mwingine wa uwazi huo. Maeneo ambayo ngiri huweza kutokea ni pamoja na:

 • Tumboni
 • Kifuani
 • Eneo la kinena
 • Korodani
 • Eneo lililowahi kufanyiwa upasuaji
 • Eneo la juu ya paja

Ngiri ni tatizo linalowasumbua watu wengi duniani na hutokea kwa jinsia zote katika umri wowote.Ngiri hupewa majina tofauti na jina hutegemea na sehemu ya mwili ambapo ngiri imejitokeza.Aina tofauti za ngiri hutibiwa tofauti kutokana na sehemu iliyopo na sababu nyingine za kitaalamu.

  Aina za ngiri

1.Ngiri kavu(inguinal hernia)-Aina hii ya ngiri huwapata watu wa jinsia zote na inapotokea kwa mwanaume huitwa ngiri ya mfuko wa korodani (scrotal hernia) na kwa mwanamke huitwa ngiri ya juu ya paja (femoral hernia).Hii ndiyo aina ya ngiri ambayo huwasumbua watu wengi zaidi na mara nyingi hutokea kwa wanaume kwa sababu wana uwazi mdogo kwenye misuli ya kinena ambao hupitisha ateri,veni na mrija wa mbegu kuelekea kwenye korodani.Uwazi huo huweza kupitisha utumbo au mafuta na kusababisha uvimbe ambao waweza kusababisha maumivu wakati wa kukohoa,kuinama au kunyanyua vitu vizito. Ngiri kavu huanza kama uvimbe mdogo ambao huongezeka kadri muda unavyozidi kwenda na huweza kuenea kutoka kwenye kinena hadi kwenye korodani zenyewe.Uvimbe huu huweza kupotea kwa kulala na kurudi pale ambapo mwili ukianza shughuli. 

2.Ngiri ya kitovu (umbilical hernia)-Aina hii ya ngiri hutokea pale ambapo utumbo au mafuta hupenyeza  kupitia sehemu dhaifu ya misuli iliyopo chini ya kitovu. Aina hii ya ngiri husababishwa na mambo makubwa matatu ambayo ni kasoro ya kuzaliwa,shinikizo la mgandamizo wa hewa ndani ya tumbo na kasoro upande wa juu wa kitovu karibu na mstari wa kati wa tumbo. Dalili ya kwanza ya ngiri ya kitovu pindi mtoto anapozaliwa ni kuwa na kitovu kirefu sana ambacho huungana na kondo la nyuma la mama ili kupeleka lishe na hewa ya kwa mtoto pindi anapokuwa ndani ya mfuko wa uzazi.

Aina hii ya ngiri huweza kumsababishia mtoto mchanga maumivu makali hivyo hulia kila wakati.Mtoto hatakiwi kufanyiwa upasuaji kwani aina hii ya ngiri huisha yenyewe miaka miwili hadi mitatu baada ya mtoto kuzaliwa,lakini kama haikuisha baada ya muda huo ndipo mtoto atatakiwa kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha tatizo hilo.

3.Aina zingine za ngiri ni pamoja na:

 • Ngiri maji(hydrocele)
 • Ngiri ya kwenye kifua(hiatus hernia)
 • Ngiri ya sehemu ya haja kubwa(anal hernia)
 • Ngiri ya tumbo(abdominal hernia)

 Je, tatizo la mshipa wa ngiri husababishwa na nini?

Vitu vinavyoweza kusababisha mtu apate ugonjwa ma mshipa wa ngiri ni pamoja na:

 • Kunyanyua vitu vizito
 • Unene wa kupindukia
 • Kikohozi cha mara kwa mara
 • Kujikamua kwa nguvu wakati wa haja kubwa kutokana na choo kuwa kigumu
 •   Korodani zisizoshuka
 •   Kuvimba kwa tezi dume
 • Lishe duni
 • Uvutaji wa tumbaku.

Tiba ya tatizo la mshipa wa ngiri.

Njia inayoweza kutatua tatizo la mshipa wa ngiri ni kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu ambazo zimelegea. Pia kutegemeana na kisababishi na aina ya ngiri mtu unaweza kufanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi. Matunda huupa mwili Vitamini C ambayo husaidia kuunganisha misuli na tishu zilizolegea na pia huharakisha kupona kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji. Kama tatizo ni kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara ni bora kusitisha uvutaji nah ii itasaidia kupunguza madhara au makali ya ngiri.

5 thoughts on “Ujue ugonjwa wa mshipa wa ngiri (hernia) na matibabu yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show