Je, upo katika hatari ya kupata saratani ya mfuko wa uzazi? Jifunze nasi!

karibu tujuzane!

Unafahamu nini kuhusu saratani ya kizazi?

Saratani ya kizazi ijulikanayo pia kama saratani ya mji wa mimba ni aina ya saratani ambayo huanza katika mfuko wa uzazi wa mwanamke (uterus) ambapo ukuaji wa mtoto wakati wa ujauzito hutokea. Aina hii ya saratani huathiri kuta za mji wa mimba pia endapo ikichelewa kugundulika huweza kuhatarisha maisha

fahamu zaidi kuhusu...

Visabishi na vihatarishi.

Mpaka sasa tafiti hazijaweza kueleza kwa undani kuhusu visababishi vya saratani ya kizazi lakini tafiti zinaonyesha kuwa mabadiliko katika jeni za seli (mutations) hupelekea seli za kawaida za mji wa mimba kubadilika na kuwa seli za saratani. Pia tafiti zimeweza kuonyesha vihatarishi ambavyo huweza kusababisha saratani ya kizazi, vihatarishi hivyo ni pamoja na;-

Mabadiliko katika msawazo wa homoni za kike

mabadiliko ya homoni za estrojeni na projesteroni hupelekea mabadiliko katika kuta za kizazi. Magonjwa au tatizo lolote ambalo linaweza kusababisha kiwango cha homoni ya estrojeni kikawa juu wakati kile cha projesteroni kikawa chini huongeza hatari ya kupata saratani ya kizazi.

Kuwa umri mkubwa

tafiti zinaonyesha kuwa kadri umri unavyoongezeka hatari ya kupata saratani ya kizazi huongezeka pia

Kuwa na uzito mkubwa (obesity)

pia kuwa na uzito mkubwa huongeza hatari ya kupata saratani ya kizazi kwani uzito mkubwa hupelekea mabadiliko katika msawazo wa homoni ya estrojeni na projesteroni.

ujauzito

Pia wanawake ambao hawajahi kuwa wajawazito katika maisha yao wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya kizazi

tuelimishane zaidi...

Dalili za saratani ya kizazi

  • Kuvuja damu ukeni (vaginal bleeding), kuvuja damu kusiko kwa kawaida  yani damu kutoka nyingi kupita kiasi wakati wa hedhi au kutoka damu katikati ya mzunguko wa hedhi au kwa wanawake ambao hedhi ilishakoma (menopausal) huweza kuwa ni dalili ya mwanzo ya saratani ya kizazi.
  •  Udhaifu wa mwili na kuwa na maumivu chini ya kitovu na sehemu ya chini ya mgongo.
  • Kupata shida na maumivu makali wakati wa kutoa haja ndogo au maumivu wakati wa tendo la ndoa.
  • Kupoteza uzito ndani ya kipindi kifupi.

Matibabu

Kama ilivyo kwa aina nyingine za saratani, saratani ya kizazi inapogundulika mapema ni rahisi zaidi kupata tiba ya uhakika.

Je, nifanye nini kupunguza hatari ya kupata saratani ya kizazi.

Kwa kuwa uzito wa mkubwa huongeza hatari ya kupata saratani ya kizazi hivyo basi kama una uzito mkubwa basi hakikisha unapunguza uzito kwa kula chakula chenye kiasi kidogo cha wanga, pia  weka ratiba ya kufanya mazoezi mara kwa mara kila wiki. Pia ni vyema kujenga tabia ya kwenda hospitali mara kwa mara kuangalia afya yako.

MEDICAL STUDENT|DMer|Entrepreneur|Tech enthusias|Aspiring Surgeon

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.