Je nini husababisha shinikizo la damu?

Shinikizo la damu hutokea wakati damu inatiririka kupitia mishipa na kusababisha mgandamizo ambao ni mkubwa kuliko ule wa kawaida katika kuta za mishipa ya damu.

Zifuatazo ni sababu zinazoweza kupelekea kupata ugonjwa wa shinikizo la damu…

  • Kuto kufanya mazoezi katika kiwango kinachotosheleza
  • Kutumia chakula chenye kiwango kikubwa cha mafuta hasa yanatokana na wanyama
  • Kuwa na uzito mkubwa wa mwili
  • Historia ya familia kuwa na shinikizo la damu
  • Matumizi ya tumbaku
  • Msongo wa mawazo
  • Matatizo ya figo
  • Matatizo ya homoni

Joseph Paul MD5

Aspiring Cardiologist ❤

All author posts

Privacy Preference Center