Majeraha ya moto

Huduma ya kwanza ili kuweza kumsaidia aliyeungua moto:

  • Mwondoe kutoka kwenye chanzo cha moto. Mweke sehem salamana yenye hewa ya kutosha.
  • Haraka mwaga maji safi juu ya ngozi iliyoungua kwa dakika 10 mpaka 15. Au tumia nguo safi uliyoilowesha kwenye maji safi kukanda sehem iliyoungua.
  • Kufanya hivi kunasaidia kupooza, kupunguza maumivu na kusafisha ngozi.
  • Kwa majeraha makubwa ya moto epuka kuingiza kidonda kwenye maji baridi kwasababu maji haya yanaweza kushusha sana joto la mwili kiasi cha kuhatarisha maisha.
  • Mvue vitu vya kubana kama pete, mkanda, saa na vitu vingine vilivyopo karibu na sehem alizoungua. Wahi kabla hazijaanza kuvimba
  • Usiondoe nguo zilizogandia kwenye vidonda au kuungulia kwenye mwili.
  • Usipasue malengelenge yaliyojitokeza baada ya kuungua.
  • Inua sehem aliyoungua juu zaidi ya usawa wa moyo. Kama ameungua kwenye mikono au miguu.
  • Funika eneo la jeraha na kitamba safi.
  • Muwahishe kwenye kituo cha afya au hospitali iliyo karibu na wewe. Na wakati mnaelekea hospitali au kituo cha afya, mpe maji ya kunywa kidogokidogo kila baada ya mda mfupi kama yuko macho na ana fahamu zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center