Huduma zipi hutolewa na daktari wa meno?

Daktari wa meno ni mtaalamu wa magonjwa ya kinywa na meno, aliyebobea katika kufanya uchunguzi, vipimo na matibabu ya magonjwa mbalimbali ya kinywa na meno, inashauriwa kumuona daktari wa meno angalau mara mbili kila mwaka kwa uchunguzi wa kawaida.

 • Unafahamu matibabu na huduma unazoweza kupata kwa daktari wa
  meno?
 • Kupata ushauri juu ya namna bora ya utunzaji wa kinywa na meno
 • Uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya fizi,kinywa,meno na mataya kwa ujumla
 • Kuziba meno yaliyotoboka
 • Kusafisha meno na kufanya yavutie
 • Kutengeneza meno bandia na kupangilia meno
 • Kufanyiwa upasuaji mdogo wa kinywa na meno ikiwemo matibabu ya mifupa ya uso na mataya pamoja na kungโ€™oa meno.
 • Uchunguzi wa saratani ya kinywa na uso
 • Kutibiwa tatizo la harufu mbaya ya kinywa

Flaviana Nyatu DDS 5 ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

A happy and passionate dental surgeon.

All author posts

Privacy Preference Center