Namna ya kuzuia sukari kushuka chini kwa wagonjwa wa kisukari

 1. Sukari kushuka chini ni moja ya madhara ya pembeni yanayo wapata wagonjwa wa kisukari. Huwapata wagonjwa wanaotumia dawa aina ya Insulin (dawa ya kuchoma) na baadhi ya dawa za kunywa. Hii hutokana na mgonjwa kuwa na nguvu ya dawa kubwa katika mzunguko kuliko sukari katika damu.

Hutokea kwa sababu aidhaย 

 • Mgonjwa amekosa mlo
 • Kutumia dozi kubwa ya dawa
 • Kutofuata ushauri elekezi wa namna ya kutumia dawa

Sukari kushuka chini inasababisha baadhi ya dalili ikiwamo

 • Kutoka jasho kwa wingi bila kufanya zoezi
 • Kichwa kuuma
 • Kusikia njaa kali
 • Kuona maluweluwe
 • Kichefuchefu
 • Kupoteza fahamu

Namna ya kuzuia

 • Kutokukosa milo
 • Kunywa dawa kwa wakati na kuzingatia dozi elekezi
 • Kuonana na daktari endapo hutokea mara kwa mara

Utakapo kuwa karibu na mgonjwa wa sukari mwenye sukari ya chini kwa kutambua kupitia dalili tajwa hapo juu; ukimpatia sukari nyepesi mfano Soda, juice, glucose yaweza okoa maisha yake kama hatua ya kwanza kabla ya kufika hospitalini

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center