Dalili za malaria sugu kwa watoto

Malaria sugu ni ugonjwa unaohatarisha maisha ya mtoto. Ugonjwa huu huanza na homa kali ambayo mara nyingi huambatana na kutapika. Ndani ya siku 1-2 watoto hudhoofika haraka na huweza kupatwa dalili zifuatazo:

  • malaria kupanda kichwani
  • kushindwa kukaa au kunywa
  • degedege
  • upungufu sugu wa damu
  • kupumua kwa shida na pamoja
  • kupungukiwa sukari mwilini
  • Ukiona dalili hizi, ni vyema kumuwahisha mtoto katika kituo cha afya kilicho karibu nawe.