Je wajua muda sahihi wa kumnyonyesha mtoto na faida zake?

Shirika la Afya Duniani WHO linashauri mtoto kuanzwa kunyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa. Huku akiendelea kunyonya maziwa ya mama pekee bila kuchanganyiwa kitu chochote kwa muda wa miezi 6. Mtoto anatakiwa anyonye kila anapohitaji mara nyingi iwezekanavyo. Baada ya hapo kumuanzishia vyakula laini kama uji, mtori huku ukiendelea kumyonyesha mpaka akifikisha umri wa miaka 2. Baada ya hapo unaweza kumuachisha kunyonya.

Utafiti unaonyesha kumyonyesha vizuri mtoto husaidia kumpa kinga dhidi ya magonjwa kama Kuhara, Pneumonia na hata magonjwa ya allergy kama Pumu.Β Pia husaidia mtoto kujenga mahusiano mazuri na mama. Utafiti uliofanyika Denmark unaonyesha kumyonyesha mtoto kunahusiana na kuongea ka kwa uweze wa mtoto kiakili(IQ).

Kwa mama kumyonyesha mtoto husaidia kuimarisha afya ya mama. Kumsaidia kurudi kwenye hali yake ya mwanzo kabla ya ujauzito. Pia huchelewesha mama kupata mimba hivyo kutumika kama njia ya uzazi wa mpango.

Nyonyesha mtoto kwa afya ya mama na mtoto.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center