TATIZO LA KUHARA KWA MTOTO

Jinsi ya kutambua mtoto anayeharisha:

Mtoto atakua anapata haja kubwa iliyo nyepesi kuliko kawaida yake na mara nyingi kwa siku kuliko kawaida yake(zaidi ya mara tatu kwa siku)

Ni sababu zipi humplekea mtoto kuharisha?

1.Maambukizi ya vimelea kama

a)Virusi. Virusi vinaongoza kwa kusababisha tatizo la kuharisha. Mfano ni Rotavirus

b)Minyoo. Minyoo husababisha kuharisha ambako ni sugu na huambatana na homa na kupungua maji mwilini. Mfano wa minyoo hyo ni Giardia na Cryptosporidium

c)Bacteria. Bacteria pia husababisha kuharisha japo kwa asilimia chache ukilinganisha na virusi. Mfano wa bacteria hao ni Campylobacter, Salmonella, Shigella.

2.Tatizo kwenye utumbo mwembamba kama kujikunja. Hii huambatana na kutapika.

Muonekano wa mtoto mwenye tatizo la kuharisha

Mtoto akiharisha kwa mda mrefu hupungukiwa maji na huonekana kama;

a)Mdomo huwa mkavu

b)Macho huingia ndani

c)Ngozi kurudi taratibu baada ya kuvutwa

d)Mkojo kutoka kidogo sana au usitoke kabisa

Dalili nyingine; Mapigo ya moyo kwenda mbio, kupumua kwa haraka, kupoteza fahamu, uchovu, upungufu wa mwili..

Ripoti kituo cha afya cha karibu yako mara baada ya kuona dalili hapo juu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center