Moyo na mzunguko wa damu

Mfumo wa mzunguko wa damu umeundwa na vitu vikuu vitatu; Moyo,mishipa ya damu na damu. Hivyo basi moyo ni muhimu kama ifuatavyo:

-Moyo hufanya kazi ya kusukuma damu katika mwili wa mwanadamu kuelekea sehemu mbali mbali za mwili.
-Damu hiyo huwa inabeba vitu vikuu vifuatavyo inapozunguka katika mwili wa mwanadamu; oksijeni,homoni,virutubisho mbalimbali na takamwili.

-Damu chafu ikisukumwa kutoka katika moyo huelekezwa kwenye mapafu ambapo mbadilishano wa hewa chafu(kabonidaioksaidi) kutoka sehemu mbalimbali za mwili na hewa safi(oksijeni) iliyopo kwenye mapafu na kusambazwa mwilini kwa ajili ya matumizi
-Pia damu inapopita katika viungo vingine vya mwili inasafirisha vitu vingine kama virutubisho,homoni na takamwili kama nilivyotaja hapo awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center