Zijue dalili kuu kumi(10) za magonjwa ya moyo na shinikizo la damu

Mara nyingi dalili za magonjwa ya moyo hutokea pale ambapo moyo unashindwa kusukuma damu kwa kiwango kinachotakiwa katika sehemu mbalimbali za mwili au mishipa ya damu inapokua imeziba au kupungua kipenyo chake hivyo kushindwa kuruhusu kiwango sahihi cha damu kupita.
Mtu mwenye magonjwa ya moyo anaweza kua na dalili mojawapo kati ya zifuatazo ambazo zinaweza ambatana na kipimo cha pressure (blood pressure) kuwa juu;

1.Kupumua kwa shida na mapigo ya moyo kwenda kasi baada ya kazi ndogo au hata ukiwa umepumzika.
2.Maumivu ya kifua
3.Kikohozi kisichokwisha
4.Maumivu ya kichwa yasiyojulikana chanzo chake hasa upande wa nyuma
5.Kujisikia uchovu na kizunguzungu
6.Kujisikia kichefuchefu na kutapika
7.Kuvimba miguu, na tumbo na wakati mwingine mishipa ya shingo kutokeza nje
8.Maumivu makali ambayo husambaa yakitokea kifuani kuelekea kwenye taya, shingo, bega na mkono wa kushoto.
9.Kutokwa na jasho kwa wingi sana mwilini
10. Pia mtu anaweza poteza fahamu

Endapo utaona dalili mojawapo ya hizo ni vema kumuona daktari kwa vipimo na matibabu zaidi na pia kujenga tabia ya kupima pressure (blood pressure) ili kuweza kutambua tatizo la shinikizo la damu mapema na kulidhibiti.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center