Huduma ya kwanza kwa aliyepaliwa (mtu mzima)

Ishara ya kimataifa ya kupaliwa

Kupaliwa hutokea wakati vitu kama chakula au kitu kingine chochote kinapoingia katika njia ya hewa (koo la hewa) na kusababisha kushindwa kupumua vizuri.

Mtu anapopaliwa njia ya hewa inaweza ikawa imezibwa yote au sehemu tu. Ikiwa njia ya hewa imezibwa kwa kiasi kidogo huweza kujisafisha yenyewe kwa kukohoa.
Ikiwa umeshuhudia mtu anapaliwa au kama unahisi mtu amepaliwa muulize “umepaliwa…?” ili kujiridhisha kama hana tatizo lingine tofauti.


NINI CHA KUFANYA.
Msaidie kufungua njia yake ya hewa kwa kufuata hatua nne zifuatazo:
KUKOHOA:
Ikiwa anaweza kuongea, kulia, kukohoa au kupumua, atakua na uwezo wa kufungua njia yake ya hewa kwa kukohoa. Kwa hiyo mhamasishe mgonjwa kukohoa mpaka atakapotema kitu kilichompalia. Ikiwa hawezi kukohoa na kuongea basi tatizo ni kubwa.

MAKOFI YA MGONGO:
Ikiwa kukohoa hakukusaidia basi muinamishe mgonjwa kuelekea mbele kasha tumia kisigino cha kiganja chako kumpiga makofi matano ya nguvu mgongoni katikati ya makombe ya mabega “shoulder blades” kama kuna kitu mdomoni mwambie akiteme . 

KUKAMUA TUMBO

Kama hatua iliyopita haikufanikiwa, simama nyuma ya mgonjwa, unganisha mikono yako na uweke tumboni kwa mgonjwa kati ya kitovu na kifua chake, mkono wako wa chini ukikunja ngumi. Vuta kwa nguvu ndani kuelekea juu.

MSAADA:
Ikiwa bado mgonjwa kapaliwa tafuta msaada wa kumfikisha mgonjwa hospitali ya karibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show