Huduma ya kwanza kwa mtoto aliyepaliwa

Kupaliwa ni hali ya kukabwa na kitu kwenye koo la hewa, hali hii huweza kujitokezaย  pale ambapo chakula au kitu chochote ambacho mtoto alikuwa anakichezea mdomoni na hatimaye kikaenda kukwama kwenye koo la hewa.

kwa mtoto mwenye umri wa zaidi ya mwaka mmoja:

Mpige makofi matano nyuma katikati ya mgongoni kwa kutumia kisigino cha mkono wako. Wakati huu mtoto unaweza ukawa umemlaza, umemkalisha au amepiga magoti.

Ukiona bado mtoto kapaliwa, simama nyuma ya yake kisha kunja ngumi na mkono mmoja, uweke kwenye tumbo karibu na kifua ukifatiwa na mkono wako mwingine kama picha inavyoonyesha hapo chini, kisha vuta kwa ndani na kuachia mara tano. Kitaalamu inajulikana kama heimlich manouver.

Kama mtoto bado kapaliwa, mfungue mdomo na chunguza kinywa chake kama kuna kitu chochote kinachomzuia kuhema na kinaonekana ukitoe.

Kama mtoto anakohoa mhimize aendele kukohoa, kwani hii ni namna ambayo mwili wenyewe unakuwa unajaribu kutoa kilichompalia.

Ukiwa bado na kama ikikulazimu, rudia hatua hizi tena kwa kuanza upya na kumpiga makofi ya mgongoni kama ilivyoelezwa hapo awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center