Jinsi ya kuhudumia wagonjwa waliopata mshtuko wa moyo.

Je, waweza vipi kutambua kuwa mtu aliyekaribu yako amepata mshtuko wa moyo?

Huwa tunaangilia vitu vitatu vya msingi;

1. Huyu mtu ameanguka ghafla na amepoteza fahamu.

2. Huyu mtu anakuwa hapumui.

3. Mtu kama huyu huwezi kusikia mapigo yake ya moyo.

Watu wengi huwa hupigwa na butwaa na kushikwa na woga wanapokumbana na hali hii. Kuna vitu mtu wa karibu anaweza kufanya kusadia kuokoa maisha ya mtu aliyepatwa na tatizo hili.

1. Hakikisha umemlaza mgonjwa kwenye sakafuni,mlaze chale. Usimlaze sehemu kama kitandani au sehemu inayobonyea.

2. Weka mikono yako kifuani katikati kuelekea kushoto ambapo moyo ulipo kwa mgonjwa kama unavyoona kwenye picha juu.

3. Bonyeza kwa nguvu , bonyeza mara 30 halafu mpe pumzi mara 2. Pumzi unampa kwa njia ya mdomo.Puliza mpaka uone kifua kimetanuka. Pumzi zigawiwe baada ya sekunde 6.

3. Fanya hili tendo kwa dakika mbili kisha badilishana na mtu mwengine. Kabla ya kubadilishana hakikisha unaangalia mapigo ya moyo sehemu hii;

4. Wakati mkiwa mnafanya hivi mmoja wenu anakuwa anawasaliana na wauguzi au ukiwa mnampeleka mgonjwa kwenye kituo cha afya.

Ukifanya hivi vitu hapa, huweza kuokoa maisha ya watu wengi. Wagonjwa wengi ambao huwa hufariki kutokana na mishtuko wa moyo ni kwasababu wengi tunakuwa hatuna ujuzi wa kutoa huduma ya kwanza kwa tatizo hili. Hizi mbinu zaweza kukusaidi kuokoa maisha mengi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center