Unajua ni kwa nini inatubidi tufanye mazoezi?

Wengi wetu tunafahamu sababu chache za kufanya mazoezi;zile ambazo wengi hukimbilia wapatapo nia ya mazoezi .Ila ulijua kuwa mazoezi yana faida nyingi Zaidi za kutupa motisha Zaidi ya kuyafanya? Zifuatazo ni baadhi ya sababu ya sisi kufanya mazoezi:

1. Mazoezi hutufanya tusijisikie vizuri, pale tunapofanya kwa kiwango sahihi na mazoezi sahihi. Hii ni kwa sababu mazoezi yanasababisha utolewaji wa kemikali zinazotufanya kujisikia vizuri na kutupa nguvu Zaidi.

2. Mazoezi yanatusaidia kupata usingizi mwororo pale yanaposaidia katika utendaji kazi mzuri wa ubongo kwa kusaidia mfumo wa damu.

3. Husaidia pia kupunguza msongo wa mawazo na kuongeza kujithamini na kujiamini kwa mtu

4. Hutupa furaha ya hali ya ukamilishaji wa jambo na kufikia malengo,pata taswira ya mtu anayepanga kuruka Kamba raundi mia moja na anaweza hii ni furaha ndani yake na yote ni kwasababu ya mazoezi.

5. Hutusaidia kuwa na muonekano mzuri na uzito sahihi unaorandana na urefu wetu pia.

6. Mazoezi yanatusaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya kudumu kama kisukari na shikinizo la damu kwa kutupa uzito sahihi na kupunguza mafuta mwilini Zaidi kusaidia mfumo wa damu.

7. Husaidia kufanya mifupa imara hadi uzeeni kwa mazoezi rahisi tu kama kukimbia na pia kuepusha magonjwa ya mifupa katika umri mkubwa.
Hizi ni baadhi tu ya sababu ambazo zinatupa mwanga kwanini hatuna budi kufanya mazoezi. Hivyo inabidi tujue ni mazoezi yapi yanatufaa na nini yatufaa kufanya sambamba na mazoezi.

Zaidi ya yote mazoezi hurefusha maisha yetu kwa kutupa afya nzuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show