Kutokwa na harufu mbaya mdomoni

Tatizo la kutokwa  harufu mbaya mdomoni  limekuwa likiwatatiza watu wengi sana,na limekuwa likiwafanya wenye tatizo hilo kukosa uhuru  wa kuongea na kuwafanya wajisikie vibaya,hata kuwapa shida ya kisaikolojia hivo wengine hujitenga  na makundi ya watu ili kuepusha  watu kuisikia harufu hiyo.Tatizo hili linawapata watu wa makundi yote hata wasomi na watu wenye pesa HALICHAGUI.

Utagundua vipi kama una tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni?

 • Kuambiwa na rafiki au mtu wako wa karibu au daktari wa meno
 • Kugundua mwenyewe na kujihisi
 • Kutokana na ishara wanazoonyesha watu wakati unaongea nao kama kunyanyua pua au kugeukia pembeni

Zifahamu sababu zinazoweza kusababisha mdomo kutoa harufu mbaya..

 • Usafi hafifu wa kinywa,watu wengi husahau kusafisha ulimi,wengine hawasafishi meno yote na kwa umakini
 • Kutoboka kwa meno na magonjwa ya fizi,vidonda mdomoni,kuwa na ugaga kwenye meno
 • Kula vyakula venye harufu kali kama vitunguu maji na vitunguu swaumu
 • Magonjwa sugu kama kisukari,magonjwa ya ini,kifua kikuu,figo,magonjwa ya koo na kansa ya mdomo
 • Kuvuta sigara,kunywa kahawa
 • Kinywa kuwa kikavu kwa muda mrefu,kupungukiwa na maji mwilini na pia kukaa kimya muda mrefu
 • Matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu

Ufanye nini kuepuka na  kutibu tatizo hili?

 • Kusafisha kinywa vizuri angalau mara mbili kwa siku,usisahau kusafisha ulimi
 • Epuka vyakula vyenye harufu kali,badala yake kula vyakula kama matunda na mbogamboga
 • Fatilia matibabu sahihi ya magonjwa sugu kama unayo
 • Kuacha kuvuta sigara
 • Tumia vyakula vinavyoongeza kiwango cha mate mdomoni na kutafuna big G zisizo na sukari
 • Kunywa maji ya kutosha
 • Tatizo hili linatibika muone daktari wa meno kwa msaada wa kitaalamu.

 

3 thoughts on “Kutokwa na harufu mbaya mdomoni

 1. Nashukuru kwa elimu daktari,pia tatizo hili nimelishuhudia sana kwa watu wenye mazoea ya kulala mdomo wazi ………je ni matatizo ya upumuaji yanapelekea mtu kulala mdomo wazi au ni mazoea ya kila siku ?????

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center