Michezo ni Uchangamfu wa Akili

Kupenda Michezo ni Afya, na kuingia kuicheza ni kuipenda afya yako. Michezo ni moja ya mazoezi mazuri sana si kwa mwili pekee kuufanya uchangamke na kuwa katika hali nzuri. Ila hata akili kuimarika sana kwa kitendo cha kuhusika kuicheza. Kuna aina nyingi sana ya michezo katika mazingira yetu yenye kuimarisha afya na kufanya watu wawe wachangamfu.

Uchangamfu ni tendo la kujiondoa katika hali ya msongo wa mawazo ambao ni hatari kwa afya ya akili. Ikiwa ni moja ya sababu ya Magonjwa hatarishi ya akili. Kuhusika katika michezo mbalimbali kama kucheza mpira, kuvuta kamba, kukimbia yote ni michezo imarishi ya kuufanya mwili kuwa bora na afya yenye uimara mkubwa.

Maeneo ni mengi unaweza ukafanya hii michezo baada ya kumaliza shughuli mbalimbali za siku au kabla ya kuanza siku. Ni muda mzuri sana unaoweka katika kujihusisha Katika michezo kiafya, afya kama msingi wa mambo mengine. Ni jambo lenye nguvu sana ukijihusisha katika michezo mbalimbali ili uwe katika hali ya uchangamfu wakati wote. Na akili ilo changamka ina nafasi kubwa sana ya kuwa na ufanisi mkubwa Sana katika maeneo ya utendaji kazi.

Jiunge katika makundi ya michezo, vikundi vya kukimbia ( jogging clubs), au jiwekee ratiba yako ya kufanya michezo kama hii na watu wengine kama njia mojawapo ya kukufanya uwe na uchangamfu na kujiongezea Nafasi kubwa ya kufanya mambo katika ubora. Pia faida ya uchangamfu huu unaotokana na michezo unazalisha kemikali iitwayo Dopamine inayompa mtu Hamasa zaidi ya kuendelea kufanya vitu na kuwa mtu bora katika maeneo mengine ya maisha.

Penda Mazoezi Katika michezo kwa Afya yako. Na penda michezo hii inayokupa hamasa kubwa sana Katika kukufanya imara kiafya kila siku. Afya ni utajiri wako hakikisha unailinda kwa kujihusisha katika michezo mbalimbali

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show