Mjamzito na matumizi ya dawa yasiyosahihi.

Kitu chochote anachokula/kunywa mwanamke mjamzito ndicho hicho hicho kinacholiwa na mtoto aliyeko tumboni, maendeleo ya ukuaji wa mtoto katika kipindi chote cha ujauzito vinategemea sana aina za vyakula anavyotumia mama mjamzito, na matokeo ya vyakula hivyo hayaishii tu katika kipindi cha ujauzito bali huendelea hata baada ya kujifungua pamoja na kipindi chote cha makuzi ya mtoto, hivyo mwanamke mjamzito mwenye malengo ya kujifungua salama hana budi kuchagua aina ya vitu anavyotumia kama vyakula kwa ajili ya kutunza Afya yake na Afya ya mtoto.

Miongoni mwa vitu ambavyo ni lazima mwanamke mwenye ujauzito ajiadhari navyo ni matumizi ya madawa mbalimbali. Kama inavyotambulika kuna aina mbili za madawa; dawa haramu(illegal drugs) na dawa halali(legal drugs). Dawa zote zina matokeo tofauti tofauti katika mwili wa mama mjamzito pamoja na mtoto aliyeko tumboni.

Matumizi ya dawa haramu maarufu kama dawa za kulevya zinachangia kwa kiasi kikubwa sana kuzorotesha Afya ya mama pamoja na mtoto, matumizi ya vitu kama Unga(cocaine) na marijuana ni hatari sana kwa Afya ya mjamzito, ukiongezea pombe, sigara na vinywaji vyenye kiungo cha kafeini(caffeine) huongeza hatari kwa mama mjamzito na hasahasa ni juu ya Afya ya mtoto. Miongoni mwa madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya madawa haya ni pamoja na;      

1. Uwezekano wa Kujifungua kabla ya muda(premature birth).

2.Kujifungua mtoto mwenye uzito chini ya kiwango stahiki(underweight).          

 3. Kifo cha mtoto kabla ya kuzaliwa(premature death).

4.mabadiliko ya kitabia wakati wa ukuaji wa mtoto. Hi inajumuisha tatizo kupungua kwa uwezo wa kutunza kumbukumbu(memory loss) pamoja na kiwango cha chini cha usikivu na umakini(attentiveness).              

5. Ongezeko la uwezekano wa mtoto kupatwa na magonjwa ya moyo pamoja na saratani.            

 6. Kupungua kwa kinga mwili za mama mjamzito kitu kinachomfanya mjamzito huyu kuwa katika hatari ya kupata na magonjwa mbalimbali kama kifua kikuu, saratani ya mapafu, magonjwa ya moyo, nk.

Wajawazito wanaotumia dawa haramu wanatoa nafasi kwa watoto wao wachanga kutumia vitu hivi wangali katika umri mdogo sana na bila ridhaa yao, hali hii huleta matokeo yanayochangia kupungua nguvu kazi ya Taifa letu.

Matumizi ya dawa halali(legal drugs) huwa yanakuwa na madhara mbalimbali pindi yanapotumia pasi na kuzingatia maelekezo sahihi ya matumizi ya dawa, madhara halisi ya matumizi ya madawa haya kwa wajawazito hayatambuliki wazi kutokana na kutokuwepo kwa tafiti nyingi juu ya matumizi ya madawa haya kwa wajawazito, lakini uwepo wa maduka mengi ya dawa muhimu umefanya upatikanaji wa dawa kuwa rahisi sana, hali hii imefanya watu kuwa na tabia ya kujinunulia na kutumia dawa kulingana na wanavyojisikia bila kupata kibali maalumu, lakini si vyema kwa mama mjamzito kutumia dawa kutoka katika maduka ya dawa muhimu bila kupata maelekezo kutoka kwa Daktari wake. Kila dawa inamfumo wake wa utendaji kazi kulingana na dozi iliyotolewa kwa kuzingatia hali ya mwili, hivyo ili kuhakikisha ujauzito unakua salama mama mjamzito anapaswa kutembelea vituo vya Afya(maternal clinic) ili kupata maelekezo yote muhimu ikiwemo maelekezo sahihi ya juu ya matumizi ya dawa mbalimbali ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi mabaya ya dawa.

Tujifunze kuzingatia kanuni bora za Afya kutokàna na maelekezo yanayotolewa katika vituo vya Afya katika kipindi chote cha ujauzito ili kuepuka kuviadhibu vichanga vyetu kwa kuvigawia vitu visivyostahili.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center