Namna sahihi ya kupiga mswaki

Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku baada ya chai na baada ya chakula cha usiku
Tumia dawa ya meno yenye madini ya fluoride
Badili mswaki kila baada ya miezi mitatu
Muone daktari wa meno mara kwa mara kwa uchunguzi na matibabu ya mapema

HATUA ZA KUPIGA MSWAKI.
1.Weka mswaki wako katika degree 45 na meno yako ili mswaki wako ugusane na meno yako pamoja na fizi.

2.Sugua sehemu ya nje ya meno yako 2-3 taratibu bila kutumia nguvu kwa mwendo wa kuzungusha kisha sogea kwenye meno mengine 2-3 na rudia ivo ivo

3.Endelea vile vile kwa meno ya ndani, mswaki ukiwa kwenye degree 45 na meno yako kwa mwendo wa kuzungusha mbele na nyuma kwenye meno na fizi zote.

4.Geuza mswaki wako nyuma ya meno ya mbele kisha kwa mwendo wa kwenda juu na chini safisha meno hayo vizuri.

5.Weka mswaki wako kwenye sehemu ya meno ya kutafunia na kwa taratibu safisha sehemu hizo kwa mwendo wa kwenda nyuma na mbele.

6.Malizia kwa kusafisha ulimi vizuri.

4 thoughts on “Namna sahihi ya kupiga mswaki

 1. habari daktari, ujumbe mzuri sana unaohitaji watu kufahamu kwa ajili ya afya njema ya vinywa vyetu. Kwa hilo shukrani.
  Kwa kuongezea ni labda ushauri tu wa jinsi ya kufanya hii elimu iwafikie watu zaidi nadhani mngetengeneza video ingesaidia sana kuelewesha. Mimi huwa nilikereketwa na magonjwa ya meno na nikaunda ujumbe kama huu ambao nadhani DaktariMkononi mnaweza kuuboresha na kuuendeleza zaidi:

  HABARI, IMEKUWA NI KAMA JAMBO LA KAWAIDA KUPIGA MSWAKI ASUBUHI. ILA WENGI WETU TUNAKOSEA JINSI YA KUPIGA MSWAKI VIZURI. PIA WENGI TUNAPIGA MARA MOJA TU ASUBUHI, ILA KIUKWELI INABIDI HADI MARA MBILI ANGALAU YAANI ASUBUHI NA USIKU KABLA YA KULALA.

  Kumekuwa na ongezeko kubwa la tatizo la meno kwa watoto na watu wazima. Wanasema ukimuelimisha mwanamke umeielimisha jamii. Ili kulinda afya zetu na za familia basi ni vizuri kuanza kufanya japo hiki kidogo ila kina mrejesho mkubwa sana.

  MENO NI SEHEMU MUHIMU YA MWILI HIVYO NI MUHIMU KUITUNZA PIA. VIDEO HIZI ZITAKUFUNDISHA KAMA UKIWA NA MOYO WA KUJIFUNZA NA KUSAIDIA FAMILIA NA RAFIKI ZAKO ASANTE SANA.

  https://www.youtube.com/watch?v=P0TJDqcRKD0

  https://www.youtube.com/watch?v=agUzXfjM_Q8&t=105s

  https://www.youtube.com/watch?v=fHXOPun1cOs

  https://www.youtube.com/watch?v=Z_7bBppIINc

  https://www.youtube.com/watch?v=cuN13xoEurE&t=19s

  KAMA WANAWAKE/WASICHANA WOTE WATAFAHAMU HAYA BASI FAMLIA ZOTE ZITAKUA NA AFYA NJEMA YA KINYWA NA MENO.

  KUWA MWANZO WA MABADILIKO HAYA

  ASANTE BARIKIWA

  ———————————————-

  Ujumbe wenyewe ndo huo ila video ni za kiingreza ila dm naamini mna uwezo wa kutengeneza za kiswahili ili ziwafikie watu wa chini kabisa pia hii tovuti inabidi itangazwe zaidi maana ujumbe ,muhimu kama huu inaonekana haujasomwa na watu wengi kama ilivotakiwa.

  Asante, endeleeni kuelimisha jamii nna mawazo mengine kama ni sawa naweza kuchangia pia.

   1. Asante sana Dr.Nyatu kwa kuelimisha jamii hasa katika masuala ya afya ya meno. Kwa upande wangu nimejifunza mengi na nitajitahidi kuyafanyia kazi nione matokeo yake

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show