Dalili za hatari wakati wa ujauzito

Wakati wa ujauzito, wakinamama hupata mabadiliko mengi kwenye miili zao. Hali ya mimba huwaweka wakinamama kwenye hatari ya aina nyingi na ndiyo maana ni muhimu kuhudhuria kliniki kwa muda muafaka.

Ni muhimu kwa hao kinamama kujua dalili za hatari wakati wa ujauzito kwasababu hizo dalili huwaweka kinamama na mtoto tumboni kwenye hatari na huweza kupoteza maisha yao.

Dalili za hatari ni:
kuona damu katika sehemu za siri au kutoka kwa uchafu yenye harufu mbaya kwenye sehemu za siri.
Kuhisi kama mtoto tumboni ameounguza kucheza au hajacheza kabisa kwa mda uliozidi siku mmoja
Kuona miguu yote miwili imevimba na pia kupata matatizo kuona au kuona giza na kupata maumivu makali ya kichwa
Kupata maumivu makali tumboni
Kupasuka kwa chupa cha maji

Kama dalili hata mmoja iliyotajwa hapo juu yakitokea, ni muhimu kuwahi kuenda katika kituo cha afya ya karibu kwaajili ya tiba. Mama hashauriwi kutumia dawa za miti shamba au dawa ya aina yoyote zaidi na zile alizozipewa na daktari.
Ni muhimu pia kwa kina baba kuzijua hizo dalili ili kuweza kumsaidia mama na kuwahisha kuenda hospitalini.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center