Kwanini haishauriwi kunywa pombe wakati wa ujauzito.

Imekuwa desturi kwa wamama wengi wajawazito kutumia pombe.Pombe ni sumu kwa mtoto tumboni na pale mama atumiapo huenda moja kwa moja kwenye mzunguko wa damu ya mtoto na kuleta athari kwenye ukuaji wa viungo vyake mbalimbali.

Haijulikani kwa hakika ni kiasi gani cha pombe ni salama kwa makuzi sahihi ya mtoto tumboni, Hivyo wataalamu hushauri kuacha pombe kabisa wakati wa ujauzito.

Madhara mbalimbali yanayoletwa na unywaji wa pombe wakati wa ujauzito ni kama yafuatayo:-

•Mimba kutoka/ kuharibika
•Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo
•Ukuaji mmbaya wa mtoto akiwa tumboni na baada ya kuzaliwa
•Mtoto kuwa na kichwa kidogo kuliko kawaida
•Mtoto kushindwa kuwa na ubongo ufanyao kazi vizuri
•Matatizo ya moyo kama tundu la moyo
•Matatizo ya figo
•Matatizo ya macho
•Matatizo ya pua
•Mtoto kuwa na matatizo ya kimaumbile ya sikio na kutosikia vizuri

Hivyo basi, ni vyema kwa wamama wote kujitahidi kutokutumia pombe wakati wa ujauzito kwa ajili ya ukuaji mzuri wa mtoto.

1 thought on “Kwanini haishauriwi kunywa pombe wakati wa ujauzito.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center