Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa ujauzito

1.Chakula bora Wanawake wajawazito, kama watu wengine, wanahitaji mchanganyiko wa protini,mbogamboga,matunda, na wanga. Pia wanapaswa kula mara nyingi zaidi, wakipata vyakula vidogo vidogo kati ya milo ya kawaida siku nzima. Vyakula mchanganyiko hulinda afya ya mama na mtoto.
2.Zuia upungufu wa chembe nyekundu za damu (anemia) Anemia (upungufu wa chembe nyekundu kwenye damu) hutokea kipindi cha ujauzito. Husababisha kujisikia uchovu,kizunguzungu, mara kwa mara. Anemia ni hatari zaidi hasa kwa akinamama wajawazito kwa sababu inaweza pelekea kujifungua kabla ya mda,na kupata mtoto mwenye uzito mdogo.Wakati wa kujifungua damu nyingi hupotea hivyo kama mama hatokua na damu ya kutosha inaweza pelekea matatizo makubwa kama kifo. Zuia anemia kwa kula vyakula vyenye protini na wingi wa madini chuma, na pia kutumia dawa ya kuongeza madini chuma mwilini.Vyakula vyenye madini ya chuma ni kama nyama,maini,maharage,mayai, nk.
3.Asidi ya foliki Ukosefu wa asidi ya foliki (au vitamini ya foleti) kunaweza kusababisha hitilafu katika uumbaji wa mtoto na hata ulemavu(mgongo nje). Tumia dawa za kuongeza madini chuma mwilini ambazo zinajumuisha asidi ya foliki, au dawa za kuongeza foliki mwilini.
4.Kupumzika.
Mama mjamzito anahitaji kupewa mda mwingi wa kupumzika hasa pale mimba inapokua kubwa kwasababu uzito unakua mkubwa na kumuelemea.Kazi nzito kama za kuinama anahitaji kusaidiwa na ndugu wa karibu.
5.Epuka Matumizi ya Bidhaa Hatari Mama mjamzito anapaswa kuepuka vitu vifuatavyo kwa sababu huhatarisha afya ya mtoto hata ikampelekea ulemavu au kifo.Vitu hivyo ni kama
1.kuepuka matumizi ya sigara au kukaa karibu na mtu anae vuta sigara
2.Kuepuka kunywa pombe
3.kuepuka kutumia madawa ya kulevya kama kokein,heroine,kutumia bangi na mirungi
6.Kuhudhuria kliniki. Mama mjamzito anahitaji kuhudhuria kliniki kila baada ya kipindi flani ili kuweza kujua hali ya mtoto tumboni.Pia wakati akihudhuria kliniki atapewa chanjo za magonjwa kama ya pepo punda,tetenas,nk.Pia hupewa dawa za kuzuia malaria wakati wa ujauzito,na dawa za kuongeza chembe nyekundu ya damu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center