Ukweli kuhusu saratani ya titi

Kila uvimbe wa titi ni saratani
UKWELI: Zaidi ya asilimia tisini ya uvimbe katika titi huwa si saratani huhitaji kipimo kudhibitisha.

Mwanamke wa umri mdogo hawezi kupata saratani ya titi
UKWELI.Inashauriwa mwanamke katika umri wa mdogo baada ya kupata hedhi kujifanyia uchunguzi wa titi kuweza kujua uvimbe ambao si saratani,uvimbe huu huwapata wanawake katika umri mdogo.

Wanawake pekee wanaweza kupata saratani ya titi
UKWELI Hata mwanaume anaweza kupata saratani ya titi lakini hutokea mara chache ikitokea huwa hatari kuliko kwa mwanamke.

Uvimbe ni dalili pekee ya kuhisi saratani ya titi
UKWELI Kuna dalili zingine kuweza kujua saratani ya titi ; Sehemu ya titi kuingia ndani , Kubadilika kwa umbo la titi, Mabadiliko kwenye chuchu kama vile chuchu kuzama ndani, chuchu kutoa maji yasiyo ya kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center